MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 714
- 1,137
Wakati wa maandamano ya nchi za Kiarabu Marekani walichekelea sana kwa kuzitukana nchi za kiarabu kwamba hazina demokrasia. Yakaja tena maandamano ya Iran Marekani walafurahi sana kwa kuona Iran inavyopata shida kuzima yale maendeleo.
Sasa ni zamu ya Marekani, leo ni siku ya nane mfululizo watu wako barabarani, hawasiki cha mwazini, sheria za Curfew zimewekwa kwenye miji mingi lakini watu hawaelewi. George Floyd kifo chake kimechochea moto ambao unaonekana kuzimika utaidharimu pakubwa sana Marekani.
Majumba ya serikali na maduka makubwa yamechomwa moto, magari na vituo vya polisi vimechomwa moto, Ikulu ya White House kama imetekwa vile kiasi kwamba rais Trump alifichwa kwenye chumba cha shimoni baada ya kuona hali ya usalama ni tete.
Ufaransa nako jana moto umewaka kwa kumbikumbu ya kifo cha Adama Traore aliyefariki miaka minne iliyopita.
Kila nchi sasa inaunga mkono maandamano ya Wamarekani.
Hii inaweza kuwa ni African American Spring. Je Trump atakuwa na uhakika wa kurudi kwenye kiti baada ya uchaguzi mwaka huu. Kumbe hata Marekani kuna shida nyingi sana za kijamii japo hawazisemi na kuzitangaza.
Ama kweli muoshwa huoshwa.