MAREKANI: Siku moja baada ya kuapishwa, watu zaidi ya 250,000 waandamana kumpinga Donald Trump

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,276
23,223
Naam, hiyo ndiyo demokrasia ya Marekani. Huwanyamazishi wapinzani wako baada ya kuapishwa kuwa Rais, mwisho wa uchaguzi ndio mwanzo wa harakati za kisiasa. Rais Obama, pamoja na ushindi wa kishindo, alianza kuonja joto la wahasimu wake toka siku ile ile anaapishwa.

Bahati ya Obama ni kwamba alikuwa na Wamarekani wengi nyuma yake. Donald Trump kwa upande wake Wamarekani wengi hawakumpigia kura ila kulingana na sheria walizojiwekea, anayepata kinachoitwa electoral votes ndiye hutangazwa mshindi.

706BEAC8-0421-48CE-BFCF-C68AC32962AA.jpg

Huko nyuma niliwahi kuonya kuwa Wamarekani kwa kuheshimu sheria na kanuni na kwa kuwa Donald Trump alishinda hawangeweza kuzuia asiapishwe. Lakini hiyo honeymoon yake ingeisha siku anakamata Kitabu takatifu na kula kiapo. Kwa kukubali kuapa huku alikjua yako mambo yanayohitaji maelezo amewapa wapinzani wake ruhusa rasmi ya kuanza mapambano.

Siku ya leo katika majimbo yote 50 ya Marekani kuna maandamano ya Wanawake dhidi ya Urais wa Donald Trump. Mjini Washington waliojitokeza na wanaoendelea kujitokeza kwenye maandamano ni maradufu ya waliojitokeza kwenye kuapishwa kwake. Hotuba yake aliyotoa jana imezidi kuwahamasisha wapinzani kuwa hatilii maanani tuhuma zinazoelekezwa kwake.

GTY-womens-march-washington-4-jt-170121_12x5_1600.jpg

Wanawake wakiandamana mjini Washington.

06557CEF-6E66-43BA-9552-F981B6335C75_w987_s_s.jpg

Wanawake mjini Washington alikoapishwa Trump jana.

1713832_1280x720.jpg

Wanawake wakiandamana mjini Chicago!
Hiyo ni miji miwili tu Washington DC na Chicago...na hii ni ya wanawake tu bado makundi mengine.

Kwa tuliokuwepo mwaka 1972 tunakumbuka jinsi Wamarekani walivyosubiri hadi Rais Richard Nixon ameapishwa kabla ya kuanza maandamano ya kumtoa. Somo kubwa hapa ni kwamba Donald Trump hawezi kuzuia haya maandamano na jaribio lolote la kufanya hivyo itakuwa ni sawa kumwaga petroli kwenye moto.

Tutaendelea kuwapa taarifa...
 
Sawa mkuu
Nimesikia kuna watu (Watanzana wenzetu) wanawaita waandamanaji hawa cry babies au sore losers lakini kusema kweli Watanzania ni watu wa ajabu kweli kweli na nashindwa kabisa kuwaelewa. Maandamano kwa sasa yanafanyika Dunia nzima, toka London hadi Berlin, toka Sydney hadi Buenos Aires, toka Ottawa hadi Mexico City...labda ni Tanzania tu hatutashuhudia maandamano kwa sababu hatujui haki zetu.

Donald Trump ni adui wa dunia na nina hakika nchi kama Marekani iliyopigania uhuru wake kwa kumwaga damu hawawezi kumkubali fashisti Trump! Trump amekuwa kimtukana Obama stupid bila kujali kuwa hamfikii Obama kwa IQ kubwa, amemtukana mpigania haki za binadamu John Lewis kwamba ni spent force...na hii yote ni kwa sababu ya uweusi wao lakini wapo Watanzania wenzetu wanashangilia.

104095714-GettyImages-622104930r.600x400.jpg

Hawa wako nje ya jengo lake la Trump Tower wakimsubiri.
 
inaugurationobama-jpg.462356

Barack Obama akiapishwa mwaka 2009

inaugurationtrump-jpg.462359

Donald Trump akiapishwa mwaka 2017

Mambo yà siku mmoja tu. Weka akiba ya maneno yako.
 
Si kosa lako, nadhani hukuwepo mwaka 1972...!
Je unakumbuka Tea Party mwaka 2010?

image.jpg

Women march in New York City! Bado California...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huu msemo uko kwetu. Kuna mambo unaweza kulazimisha lkn mengine huwezi.
Hivi maandamano yakizidi yakimtaka aachie ngazi unadhani hataachia?
Utaongozaje watu wasiokuta uwaongoze?
Ubabe wowote ule una kikomo chake. Tuwaache wamarekani washughulike na Trump wao.
Ila waandamanaji wakae wakijua msemo usemao JOGOO AWIKE ,ASIWIKE KUTAKUCHA. WAMVUMILIE TU TRUMP
 
Hawezi kuachia kizembe. Hivi unajua hata kama yeye ni mzungu ila ana moyo na interests zake hapo.

Trump ndo rais hapo hadi miaka minne mengine porojo tu maana hata matokeo yalipotangazwa si waliandamana hao na kuanza sign sign za kupinga matokeo wameishia wapi.
Huu msemo uko kwetu. Kuna mambo unaweza kulazimisha lkn mengine huwezi.
Hivi maandamano yakizidi yakimtaka aachie ngazi unadhani hataachia?
Utaongozaje watu wasiokuta uwaongoze?
Ubabe wowote ule una kikomo chake. Tuwaache wamarekani washughulike na Trump wao.
 
Naomba niwape tu taarifa kwamba hizi harakati si za kumtoa Donald Trump madarakani, ni za kuhamasisha watu wawe tayari kwa uchaguzi wa mwaka 2018, wasifanye makosa tena. Kwa sasa Trump ana House na ana Senate na njia moja ya kumpunguzia nguvu ni kumnyima mojawpo kama si zote.

Ni kwa sababu watu wengi hawakuhangaika kujitokeza kupiga kura ndio maana alipata ushindi alioupata. Harakati hizi pia zisihusishwe na Hillary Clinton, huyo hayuko tena kwenye ramani, kinachopiganiwa nikuhakikisha haki za wote zinalindwa na uhuru wa vyombo vya habari hauingiliwi.
 
Mkuu mag3

Kuandamana ni haki yao kikatiba! Let them air their voices, and frustrations! I think the POTUS is a smart person - he will listen and calm the situation.

Hotuba ya Jana ilkua inalenga Ku unify taifa.. POTUS anajitahd sana ila DEMs r not giving him the chance to lead..DEMs seats Jana xlkua empty..it tells the story!

The guy won with a very hard fought victory..na hili ndio somo..u can still win even without the system jus believe in your self...Hillary alkr kushindwa and suggested tumpe chance!! Let's give him a chance to lead us..

Kingine mkuu umeandka kishabk mno ..
 
Nimesikia kuna watu (Watanzana wenzetu) wanawaita waandamanaji hawa cry babies au sore losers lakini kusema kweli Watanzania ni watu wa ajabu kweli kweli na nashindwa kabisa kuwaelewa. Maandamano kwa sasa yanafanyika Dunia nzima, toka London hadi Berlin, toka Sydney hadi Buenos Aires, toka Ottawa hadi Mexico City...labda ni Tanzania tu hatutashuhudia maandamano kwa sababu hatujui haki zetu.

Donald Trump ni adui wa dunia na nina hakika nchi kama Marekani iliyopigania uhuru wake kwa kumwaga damu hawawezi kumkubali fashisti Trump! Trump amekuwa kimtukana Obama stupid bila kujali kuwa hamfikii Obama kwa IQ kubwa, amemtukana mpigania haki za binadamu John Lewis kwamba ni spent force...na hii yote ni kwa sababu ya uweusi wao lakini wapo Watanzania wenzetu wanashangilia.

104095714-GettyImages-622104930r.600x400.jpg

Hawa wako nje ya jengo lake la Trump Tower wakimsubiri.
Mkuu mnaandamana kwakuwa Trump kamtukana Obama?
 
Back
Top Bottom