Marekani na South Korea wanavyokua watumwa kwa Korea ya Kaskazini

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,233
16,202
North Korea yeye alitangaza tu kuwa wamefanikiwa kulipua Bomu la haidrojen
Baada ya hapo kimya hawajaongea tena.

Baada ya muda matamko mbalimbali yakatolewa ye bado akawa kimya
Leo nasikia Marekani na South Korea wamepitisha ndege za kivita karibu na mpaka wa North Korea ili kuionyesha nguvu zao za kijeshi.

Mimi naona kama wamekua watumwa tu kwa sababu mtu amejaribu vifaa vyake amekaa kimya wao wanajishaua.

Sasa nasubiri Korea ya Kaskazini kuzungumza baada ya tukio hili walilolifanya marekakani na Korea ya Kusini.

Asipoongea basi jamaa atakua anaidharau sana marekani na south Korea
Ila naomba kuuliza why marekani anamlinda sana Korea ya kusini.

Je, ipi ina nguvu za kijeshi na vifaa kuliko nyingine kati ya North Korea na South Korea.4

Maana naona kama Korea ya Kazkazini ni masikini sana huku uchumi wake ukidaiwa ni wa hali mbaya.

Wakuu mnisaidie hapa
 
Last edited by a moderator:
Korea kusini ni mshirika mkuu wa marekani katika eneo la peninsula ya Korea amboyo ni eneo muhimu sana kijeshi (strategic area) maana USA wanaweza kuwaspy maahasimu wake akina Korea kaskazini, China,Vietnam, Russia. Marekani lazima aiunge mkono Korea kusini maana yeye ndio chanzo cha Korean war. kipindi cha vita baridi na usovieti, na akasababisha kuvunjika kwa Korea na kuazaa Korea mbili, hivyo ni lazima USA amlinde korea kusini maana Korea kaskazini walnatishia usalama wa Korea kusini.

kwa upande wa uchumi Korea kusini ina uchumi wa kibepari wanatumia mfumo wa soko huria hivyo wanauza bidhaa zao kwenye soko la dunia lakini Korea kaskazini wana uchumi wa kijamaa uchumi (closed economy) hawauzi bidhaa zao kwenye soko la dunia, ingawa inasemekanavwanauza silaha za ila ni kwa kiwango kidogo sana.

kijeshi Korea kusini ipo top ten kutokana na global power index. Kwa upande wa Korea kaskazini wao wamewekeza sana katika jeshi ingawa ni vigumu kujua uwezo alisi wa kijeshi wa Korea kaskazini kwa sababu ni taifa lenye siri na mambo mengi hayawekwi wazi. wanatumia sana chanzo kimoja cha habari ambacho ni channel ya taifa ila zaidi ya hapo ni ngumu kupata taarifa hata nchi za magharibi hawana uhakika na estimate zao kuhusu Korea kaskazini maana wanahabari wao hawaruhusiwi kuingia Korea kaskazini pia majasujii hawawezi kuingia maana wakorea kaskazini wanausiri mkubwa ndiyo maana inaonekana kuwa Korea kaskazini imejitenga na dunia
 
Korea kaskazini hawawezekani kwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na vya kusafiri. kwasababu havitaathiri chochote katika uchumi wake maana wamejitenga na dunia ya kimagharibi. may be USA, Korea kusini na Japan pamoja washirika wengine wa marekani waingilie kijeshi kusitisha uzalishaji wa mabomu ya nyuklia na hydrogen bombs.

Na wakifanya hivyo itakuwa ni vita kubwa tena yaweza kuwa ni ya kinyuklia na itaweza kuhusisha mataifa makubwa . Korea kaskazini atakuwa anaungwa mkono na China , Russia, Iran na maadhi ya washirika wa haya mataifa . Marekani na Korea kusini wataungwa mkono na Japan NATO na washirika wake.
 
Korea kaskazini hawawezekani kwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na vya kusafiri. kwasababu havitaathiri chochote katika uchumi wake maana wamejitenga na dunia ya kimagharibi. may be USA, Korea kusini na Japan pamoja wahirika wengine wa marekani waingilie kijeshi kusitisha uzalishaji wa mabomu ya nyuklia na hydrogen bombs.

Na wakifanya hivyo itakuwa ni vita kubwa tena yaweza kuwa ni ya kinyuklia na itaweza kuhusisha mataifa makubwa . Korea kaskazini atakuwa anaungwa mkono na China , Russia, Iran na maadhi ya washirika wa haya mataifa . Marekani na Korea kusini wataungwa mkono na Japan NATO na washirika wake.
china na russia hawawezi kumuunga mkono north korea kwenye vita hata kidogo iyo ilikua zaman sasa ivi china hana maslahi yoyote na north korea zaidi ya kuwatumia kama bufferzone between them and south korea kumbuka china hataki south korea na marekani wawe na kambi za jeshi karibu na mipaka yake ndo mana wameilinda serekali ya north korea kwa miaka mingi ila sasa china na north korea hawana mahusiano mazuri toka aingie raisi kim. hata kiuchumi china is south Korea's number 1 trading partner unafkiri china ataharibu mahusiano yake na south korea kwajili ya kiulinda north korea ambayo ni maskini na wanategemea misaada kutoka usa na south korea?
 
Hata sasa Urusi na China ndiyo wanayoifanya Korea kaskazini kujiamini kiasi cha kufanya majaribio. ya mabomu ya nyuklia maana wanailinda na lazima waiunge mkono Korea kaskazini. sababu ya kuiunga mkono Korea kaskazini ni kupunguza uwepo wa marekani katika eneo la peninsula ya Korea na kuondoa involvement ya marekani katika eneo la south china sea .

Kwa sasa Kama China akimchoka Kim Jong Un na sera zake za kijeshi basi hapo ndipo itakapokuwa mwisho wa Korea kaskazini. China wapo bega kwa bega na Korea kaskazini . Sababu ya kuwa nae hivyo ni ukweli kwaba Korean peninsula ni strategic area kijeshi na uwepo wa marekani katika eneo hilo kutatishia usalama wa China & Urusi.

urusi na China wanailinda Korea kaskazini kwa sababu wao ni wanachama wakudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa. Hivyo kupitia nguvu yao ya kura ya turufu (veto power) wanazuia maazimio mbalimbali ya baraza la usalama ili Korea kaskazini isiwekewe vikwazo ndo maana inapeta tuu ingawa inawekewa vikwazo na nchi za magharibi.
 
Last edited:
Hata sasa Urusi na China ndiyo wanayoifanya Korea kaskazini kujiamini kiasi cha kufanya majaribio. ya mabomu ya nyuklia maana wanailinda na lazima waiunge mkono Korea kaskazini. sababu ya kuiunga mkono Korea kaskazini ni kupunguza uwepo wa marekani katika eneo la peninsula ya Korea na kuondoa involvement ya marekani katika eneo la south china sea .

Kwa sasa Kama China akimchoka Kim Jong Un na sera zake za kijeshi basi hapo ndipo itakapokuwa mwisho wa Korea kaskazini. China wapo bega kwa bega na Korea kaskazini . Sababu ya kuwa nae hivyo ni ukweli kwaba Korean peninsula ni strategic area kijeshi na uwepo wa marekani katika eneo hilo kutatishia usalama wa China & Urusi.
ni kweli kabisa hata enzi ya korean war mmarekani alirudisha majeshi ya north korea nyuma kabisa karibu na mpaka wa china hiyo ndio sababu iliomfanya mchina aingilie kati na kumsaidia north korea baada ya china kuingilia majeshi ya marekani yalirudishwa hadi eneo ambalo leo ndio mpaka kati ya north na south korea. kiufupi bila ya china leo hii pasingekua na nchi inaitwa korea kaskazini.... north na south korea ingekua ni nchi moja tu yaani korea
 
Korea kusini ni mshirika mkuu wa marekani katika eneo la peninsula ya Korea amboyo ni eneo muhimu sana kijeshi (strategic area) maana USA wanaweza kuwaspy maahasimu wake akina Korea kaskazini, China,Vietnam, Russia. Marekani lazima aiunge mkono Korea kusini maana yeye ndio chanzo cha Korean war. kipindi cha vita baridi na usovieti, na akasababisha kuvunjika kwa Korea na kuazaa Korea mbili, hivyo ni lazima USA amlinde korea kusini maana Korea kaskazini walnatishia usalama wa Korea kusini.

kwa upande wa uchumi Korea kusini ina uchumi wa kibepari wanatumia mfumo wa soko huria hivyo wanauza bidhaa zao kwenye soko la dunia lakini Korea kaskazini wana uchumi wa kijamaa uchumi (closed economy) hawauzi bidhaa zao kwenye soko la dunia, ingawa inasemekanavwanauza silaha za ila ni kwa kiwango kidogo sana.

kijeshi Korea kusini ipo top ten kutokana na global power index. Kwa upande wa Korea kaskazini wao wamewekeza sana katika jeshi ingawa ni vigumu kujua uwezo alisi wa kijeshi wa Korea kaskazini kwa sababu ni taifa lenye siri na mambo mengi hayawekwi wazi. wanatumia sana chanzo kimoja cha habari ambacho ni channel ya taifa ila zaidi ya hapo ni ngumu kupata taarifa hata nchi za magharibi hawana uhakika na estimate zao kuhusu Korea kaskazini maana wanahabari wao hawaruhusiwi kuingia Korea kaskazini pia majasujii hawawezi kuingia maana wakorea kaskazini wanausiri mkubwa ndiyo maana inaonekana kuwa Korea kaskazini imejitenga na dunia
Asante kwa ufafanuz,je korea kaskazin ina ofis za ubaloz nchi mbalimbali duniani?je nchi nyingine zina ofis za kibaloz korea kaskazini?je Kiongoz wa Korea huenda kwenye vikao na mikutano ya UNO huko Amerika?
 
china na russia hawawezi kumuunga mkono north korea kwenye vita hata kidogo iyo ilikua zaman sasa ivi china hana maslahi yoyote na north korea zaidi ya kuwatumia kama bufferzone between them and south korea kumbuka china hataki south korea na marekani wawe na kambi za jeshi karibu na mipaka yake ndo mana wameilinda serekali ya north korea kwa miaka mingi ila sasa china na north korea hawana mahusiano mazuri toka aingie raisi kim. hata kiuchumi china is south Korea's number 1 trading partner unafkiri china ataharibu mahusiano yake na south korea kwajili ya kiulinda north korea ambayo ni maskini na wanategemea misaada kutoka usa na south korea?
So North Korea bado anasaidiwa na USA na South Korea ingawa hawaelewani?
 
ni kweli kabisa hata enzi ya korean war mmarekani alirudisha majeshi ya north korea nyuma kabisa karibu na mpaka wa china hiyo ndio sababu iliomfanya mchina aingilie kati na kumsaidia north korea baada ya china kuingilia majeshi ya marekani yalirudishwa hadi eneo ambalo leo ndio mpaka kati ya north na south korea. kiufupi bila ya china leo hii pasingekua na nchi inaitwa korea kaskazini.... north na south korea ingekua ni nchi moja tu yaani korea
Hawa jamaa ni ndugu kabisa ila ukweli ni kwamba Mabepar walifanikiwa kuwagombanisha na.mpaka leo hawajapatana ilhali ni damu moja,wangekuwa taifa moja wangekua na nguvu sana ya kiuchum na kijeshi
 
So North Korea bado anasaidiwa na USA na South Korea ingawa hawaelewani?
ndio ukweli huo. miaka ya 90 north korea ilitokea njaa kali sana walikufa watu zaidi ya million 1 kwa njaa usa china na south korea ndio walitoa msaada mkubwa wa chakula. na kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 south korea imetoa msaada wa zaidi dola billion 1.2 na usa walitoa msaada kwa makubaliano kwamba north korea itaachana mpango wake wa nuclear japo hawajaacha. south Korea pia ilipunguza misaada 2010 baada ya north korea kushambulia meli zao. kiufupi north korea wanatumia silaha za nuclear kuitisha marekani iwape misaada
 
The Korean War, 1950–1953. The Korean War began as a civil war between North and South Korea, but the conflict soon became international when, under U.S. leadership, the United Nations joined to support South Korea and the People's Republic of China (PRC) entered to aid North Korea.
Korean War - Office of the Historian
potd-south-korea_3157929k.jpg
 
Hawa jamaa ni ndugu kabisa ila ukweli ni kwamba Mabepar walifanikiwa kuwagombanisha na.mpaka leo hawajapatana ilhali ni damu moja,wangekuwa taifa moja wangekua na nguvu sana ya kiuchum na kijeshi
Wakorea ni ndugu waliotenganishwa na itikadi za kijamaa na kibepari wakati wa vita baridi. Soviet Union walikuwa wanataka Korea nzima iwe ya kijamaa na marekani nao walokuwa wanataka Korea iwe ya kibepari. malengo yakasababisha vita (Korean war) iyosababisha kugawanyika taifa la Korea.

Madhara ya ujamaa na ubepari yanaonekana hadi sasa wakorea ni ndugu ila wanaishi kwa uhasama mkubwa sana. Ingawa kuna nyakati wanandugu huvuka mpaka na kusalimiana. . Lakini mgogoro wa Korea leo hii husababishwa na Marekani maana ujamaa wa Soviet ulishakufa zamani , Sera ya marekani ndiyo inayozidisha mgogoro huu.

Inawezekana Korea kuungana na Kama ikitokea basi Korea itakuwa taifa kubwa lenye uchumi na nguvu za kijeshi. Ingawa ni ngumu Sana kutokea hivyo. Majuzi mwanadiplomasia wa Korea kaskazini aliyekuwa akishughulikia mchakato wa kuungana Korea mbili alipata ajali ya gari na kufariki dunia. Huyu aliteuliwa na Kim Jong Un asimamie mazungumzo, mawazo yangu baada ya kifo hiki huenda Kim akabadilisha maamuzi na kuzorotesha mchakato wa kuungana tena baada ya kifo hicho ndio kwanza Korea kaskazini wamejitangaza kufanya jaribio la H-Bomb. Hii itazorotesha mazungumzo na huenda ikawa ni ndoto kuungana. Ujerumani waliweza kuungana coz ujerimani mashariki ilikuwa bado haijakomaa na Sera na mfumo wa kijamaa pia kusambaratika kwa iliyokuwa Soviet Union kulisababisha iwe rahisi kuungana ujerumani. na sasa ndilo taifa lenye nguvu za kiuchumi barani ulaya na kanda nzima ya umoja wa ulaya (EU)
 
kwa wale ambao wanafatilia vizur habar za kimataifa watailewa north korea ndio mtindo wao wakiwa na hali ngumu kiuchumi huwa wana fanya nuclear test na kitishia kuanzisha vita mwisho wa siku wanapewa pesa na south korea au marekani ili waachane na mipango ya vita na nuclear na wanatulia baada ya miaka kadhaa wanarudia tena hii si mara ya kwanza kutokea.
 
Mkuu safari hii wamefanya jaribio la kwanza la H-Bomb baada ya muda mchacheuliopita Kiongozi mkuu wa Korea kaskazini ( DPRK) kutangaza kuwa wanamiliki H-Bomb na watalitumia wakati wowote kulinda sovereignty yao. Binafsi naona kuwa Korea kaskazini anacheza conspiracy theories na Marekani na Korea kusini. kuna kitu kinafichwa hapo. Pia DPRK wanawatishia wamarekani kupitia Korea kusini (maana mmarekani ana maslahi yake huko) kwahiyo mmarekani hapati usingizi na propaganda za DPRK. Mmarekani anaumiza kichwa dhidi ya DPRK ila haumizi kichwa sana dhidi ya Iran ndo maana wamefikia makubaliano na Iran kuhusu Iran Nuclear Deal
 
Asante kwa ufafanuz,je korea kaskazin ina ofis za ubaloz nchi mbalimbali duniani?je nchi nyingine zina ofis za kibaloz korea kaskazini?je Kiongoz wa Korea huenda kwenye vikao na mikutano ya UNO huko Amerika?
Mwaka 1991 DPRK (Korea kaskazini) iliijiunga na UN . DPRK wanauhusiano wa diplomatisia na mataifa machache sana Kama Italy,Germany, Philippines, Canada, UK, Mexico Australia na New Zealand. ingawa haina diplomatic mission na nchi hizi.

DPRK walikuwa na uhusiano mzuri na nchi za kijamaa wakati wa vita baridi . Ingawa ni mwanachama wa UN baadhi ya nchi haziitambui DPRK ie Ufaransa na Estonia . Ni nchi iliyojitenga na dunia baada ya kutegwa na mataifa mengi ya kibepari na kimagharibi kutokana na madai yao kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na programs za mabumu ya nyuklia baada ya kujitoa kwenye mkataba wa Nuclear Nonproliferation Treaty. Kwa upande wa Afrika sidhani Kama wana uhusiano wa kidiplomasia na nchi za Afrika.
 
Back
Top Bottom