Marekani mbioni kukamilisha dili kubwa la silaha kwa Saudi Arabia

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,417
9,603
82b403eadb86c20ef99736699c4f6e8f.jpg

Marekani ipo mbioni kukamilisha dili la silaha kwa Saudi Arabia lenye thamani zaidi ya dola billion mia moja($100B),hayo yamesemwa na afisa kwenye Ikulu ya Marekani ambaye jina lake halikutajwa.

Afisa huyo ameeleza kwamba Marekani inaweza kufanya kuongezeka uwezo wa ulinzi wa nchi hiyo ya kifalme kupita dola billioni mia tatu($300 billioni) kwa kipindi cha muongo mmoja.

Licha ya dili hilo Marekani imeeleza kwamba itahakikisha Israel inakua zaidi ya majirani zake.

Afisa huyo alieleza kwamba wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili hilo.
Haya yanajiri ikiwa ni wiki moja kabla ya ziara ya Rais mpya wa Marekani Donald Trump hapo May 19.

Marekani ndiyo muuzaji mkuu wa silaha na vifaa vingine vya kijeshi kwa Saudia, huku ufalme huo ukinunua vifaa ikiwemo ndege za kivita na vifaa vingine vya mawasiliano vyenye thamani ya makumi ya mabilioni ya dola kwa miaka ya hivi karibuni.

Wakati makundi ya haki za binadamu yakilaumu Marekani kwa usambazaji wa silaha kwa Saudi Arabia ambayo imekua ikiendeleza mashambulizi yake nchini Yemen, dili hilo kubwa linakuja wakati Trump akijaribu kutekeleza ahadi zake wakati wa kampeni za kuchochea ukuaji wa uchumi wa Marekani kupitia viwanda.

Ofisa mwingine ambaye jina lake halikutajwa alisema kwamba "Hii ni hatua nzuri kwa uchumi wa Marekani lakini pia itakua ni nzuri hasa kwenye kujenga uwezo zaidi kutokana na changamoto za eneo hilo".

Kwenye ziara yake hyo Rais Trump anatarajiwa kujadili mapambano dhidi ya kundi la kigaidi Islamic state, vita vinavyoendelea nchini Yemen na pia kuhusu Syria.

Pamoja na kutembelea Saudi Arabia, pia Trump anatarajia kuzuru Israel, Brussels,Vatican na Sicily kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa NATO.

UPDATES:

Dili ni la dola bilioni mia tatu hamsini($350bn) na si dola bilioni mia moja kama ilivyoarifiwa hapo awali.

4fbfc672172531a68715f776d2f70340.jpg
 
Aaaah, wameona isiwe nongwa wanunue makombora yote ya kuzuia mashambulizi na kufanya mashambulizi.

Haha, Kwa kweli. Na usikute Mmarekani anamwaga masilaha haya yote huku anaangalia reaction ya Iran.
 
Haha, Kwa kweli. Na usikute Mmarekani anamwaga masilaha haya yote huku anaangalia reaction ya Iran.
Eeeeh, ashajua ili amdhibiti vizuri Irani lazima Saudia wawe na siraha nzito, ili ikifika wakati mujarab basi wanapeleka wataalamu tu. Na siku Iran akianzisha nyoko, basi ujue atapigana na Israel wakiwa nyuma ya Saudia.
 
Saudia Ana kampani kubwa sana ya nchi nying za kiislam Iran akipigana na Saudia anaweza kujikuta anapigana na nchi hata 20 .....mwaka juz alifanya mazoez makubwa ya kijeshi kuwahi kutokea yakihusisha nchi zaidi 15 zinazomuunga mkono
 
Eeeeh, ashajua ili amdhibiti vizuri Irani lazima Saudia wawe na siraha nzito, ili ikifika wakati mujarab basi wanapeleka wataalamu tu. Na siku Iran akianzisha nyoko, basi ujue atapigana na Israel wakiwa nyuma ya Saudia.
Yap, Umenena!
 
Kuna stock ya makombora ya Tomahwk ilikuwa inaelekea expire date,sasa mmarekani ndo kamshikisha huyu headchopper akawamalize waarabu wenzie
What if ni kwa ajili ya kujilinda tu, usalama wenyewe wa huko ni utata, asilaumiwe kwa kweli.
 
Back
Top Bottom