Marekani kufungua ubalozi mpya leo mjini Jerusalem -

Marekani kufungua ubalozi mpya leo mjini Jerusalem -

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,401
Marekani kufungua ubalozi mpya leo mjini jerusalem

Ofis ya ubalozi ambao itahudumu kama ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem
Marekani itafunguq ubalozi wake mpya mjini Jerusalem hatua ambayo imesifiwa na Israel na kulaaniwa na Wapalestina ambao wanakusanyika kwa maandamano makubwa.
Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner.
Wengi wa maafisa kutoka Muungano wa Ulaya hawatahudhuria.
Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umegadhabisha Wapalestina amboa wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mku wa badaye.
Trump: Jerusalem ni mji mkuu wa Israel

Israel ilichukua udhibiti wa eneo la Jurusalem mashariki mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya kati, na inahutaja mji huo kuwa wake na usiogawanwa
Hatua hiyo ya Trump ya mwaka uliopita ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ilivunja msimamo wa wastani wa Marekani kwa suala la mji huo na kwenda kinyume na misimamo ya nchi zingine duniani.
Ni kipi kitafunguliwa na ni nani atahudhuria?
Ubalozi wa mdogo utaanza kutoa huduma kuanzia leo Jumatatu kwenye jengo la ofisi za ubalozi mjini Jerusalem.
Eneo lingine kubwa litatafutwa baadaye wakati ubalozi wote utahama kutoka mji wa Tel Aviv.

Sherehe za ufunguzi zilifanywa mapema ili ziweze kuenda sambamba na sherehe za miaka 70 za kuanzishwa taifa la Israel.
Rais Trump anatarajiwa kuhutubia wale ambaq watahudhuria sherehe hiyo kwa njia ya video.

Ivanka Trump akimsalimia balozi wa Marekani nchini Israel David Friedman pamoja na mumewe Jared Kushner (kulia) baada ya kuwasili Israel

Kando na Ivanka Trump na Jared Kushner ambao wote ni washauri wakuu kwenye Ikulu ya White House, Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin na naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni John Sullivan watakuwa kwenye sherehe hiyo.
Muungano wa Ulaya umepinga vikali kuhamishwa kwa ubalzo huo na mabalozi wengine wa nchi za EU hawatahudhuria sherehe hiyo.
Wapalestina wampinga Trump kuhusu Jerusalem
Hata hivyo wanadiplomasia kadhaa wa kigeni wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo waakilishi kutoka Hungary, Romania na Jamhuri ya Czech ambayo ilizuia taarifa ya pamoja ya EU kuhusu suala hilo.
Marais wa Guatemala na Paraguay pia nao wanatarajiwa kuhudhuria; nchi hizo zote mbili ziliamua kuhamisha balozi zao kwenda Jerusalem baada ya Trump kutoa tangazo hilo.

Israel imekuwa ikisherekea

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitoa wito kwa nchi zote kujiunga na Marekani na kuhamisha balozi zao kwenda Jerusalem.
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ameutaja uamuzi wa Trump kama dafrao ya karne.

Wapalestina wameandamana kupinga kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani
Maefu ya Wapalestina wanakusanyika kuandamana kwenye ua unaotenganisha Israwl na ukanda wa Gaza.
Muda wa kuhamishwa ubalozi huo umezua wasi wasi wa kongezeka msukosko huko Gaza

Tangu mwisho wa mwezi Machi zaidi ya wapalestina 40 wameuawa na wanajeshi wa Israel wakati wa maandamano ya mpakani.
Mku wa shriika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ameilaumu Isreal kwa kutumia nguvu nyingi.
Hali ya mji wa Jerusalem ndiyo chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestina.
Tangu mwaka 1967 Israel ilijenga makao mengine kwa karibu wayahudi 200,000 huko Jerusalem mashariki. Makao hayo yanatajwa kuwa haramu chini ya sheria ya kimataifa, licha ya Israel kupinga hilo.
Mada zinazohusiana
_101529930_hi046763169.jpg
_101526211_ivanka.jpg
 
Hii ni hatua muhimu sana kuukaribia mwisho wa nyakati, mwisho wa tawala za dunia na kuanza kwa UFALME WA MUNGU. Bado kidogo tutashuhudia ule mkataba wa amani uliotabiriwa na Nabii Danieli ambao utavunjika na kupelekea Jerusalemu kuharibiwa vibaya sana katika vita itakayotokea.

Biblia imeandika kila kitu. Wenye hekima zao na busara wametulia kimya wanafuatilia kwa makini sana ili ile saa itakapofika wajue ni wapi watakimbilia.

Hapa ndipo penye subira na hekima ya watakatifu! Mwenye masikio na asikie, mwenye kusoma na afahamu!
 
Vita ya wapalestina na waisrael haitamalizika mpaka mwisho wa ulimwengu
 
Trump anachofanya ni kuteka roho za wamarekani.
anajua kwa kuishikilia Israel ndo salama yake..
 
Hii ni hatua muhimu sana kuukaribia mwisho wa nyakati, mwisho wa tawala za dunia na kuanza kwa UFALME WA MUNGU. Bado kidogo tutashuhudia ule mkataba wa amani uliotabiriwa na Nabii Danieli ambao utavunjika na kupelekea Jerusalemu kuharibiwa vibaya sana katika vita itakayotokea.

Biblia imeandika kila kitu. Wenye hekima zao na busara wametulia kimya wanafuatilia kwa makini sana ili ile saa itakapofika wajue ni wapi watakimbilia.

Hapa ndipo penye subira na hekima ya watakatifu! Mwenye masikio na asikie, mwenye kusoma na afahamu!
Siku zote sijawahi kusoma eti jerusalemu iko palestina
Toka enzi na enzi nasoma jerusalemu ni ya israel
Hata bible naisoma sana lakini sijawahi kuona ni wapi imeandika jerusalem ilikuwa mjii mkuu wa palestina bali jerusalem mji mkuu wa israel toka enzi za daudi mfalme
 
Siku zote sijawahi kusoma eti jerusalemu iko palestina
Toka enzi na enzi nasoma jerusalemu ni ya israel
Hata bible naisoma sana lakini sijawahi kuona ni wapi imeandika jerusalem ilikuwa mjii mkuu wa palestina bali jerusalem mji mkuu wa israel toka enzi za daudi mfalme
Uko sahihi Mkuu; Jerusalem ni Mji Mkuu wa Israel wa NYAKATI ZOTE na ni kati ya miji michache sana ya kale ambayo bado inakaliwa na watu. Hao waarabu ukiwauliza watoe justification yoyote ni vipi Jerusalem ni mji wao wataishia tu oooh; unajua Mtume alienda sijui wapi kupitia Jerusalem; oooh; unajua (Nabii) Ibrahim alikuwa moslem; oooh; unajua (Nabii) Adam alikuwa moslem. Hakuna zaidi ya hadithi za aina hiyo. Kinyume chake kuna countless sources both religious and non-religious za tangu kale zinazoutambua Jerusalem kama wa Israel. Ukienda hata maktaba za Rumi wakati wa Roman Empire (BC), Jerusalem ilijulikana ni ya Israel.

Cc: Bandiwe, njoo na huku uendelee kueneza ujinga wako.
 
Back
Top Bottom