Kwaajili ya amani ya na maendeleo ya Somalia, Afrika na Dunia nzima, ni lazima Dunia nzima, watu wote tushirikiane kuumaliza ushenzi wa Al-Shabab. Wasomalia ni binadamu wanaotakiwa kuishi kwa furaha, amani, upendo na kuifurahia Dunia waliyopewa na Mungu lakini Al-Shabab wameondoa matumaini yote. Mimi nawalaumu Marekani, mataifa yote makubwa Duniani pamoja na AU kwa kutokushiriki kikamilifu katika jitihada za kuwaangamiza Al-Shabab. Hata kama kungekuwa na sumu au vijimelea vinavyoweza kuwaangamiza Al-Shabab pekee, mimi ningeunga mkono.