ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,603
Jaribio hili linafanyika huku kukiwa na mzozo mkubwa baina ya Marekani na Nkorea kuhusiana na silaha za nyuklia. Japo wachambuzi wengi wanaona jaribio hili ni kama kufikisha ujumbe mzito kwa Korea kaskazini, Marekani imekana jambo hilo na kusema kwamba jaribio hilo halihusiani na mzozo huo bali ni moja ya kuweka utayari silaha zake kwa ajili ya usalama wa nchi.
Minuteman III ni kombora pekee la nyuklia la Marekani ambalo linarushwa toka ardhini, lina uzito wa kilogram 35,300 huku likiwa na uwezo wa kubeba vichwa vitatu vya nyuklia vyote vikiwa na uwezo wa kulipua sehemu tofauti tofauti.Vichwa hvyo vikiwa na mlipuko wa 300-500kilotons kwa kichwa kimoja. Lina weza kwenda umbali wa hadi 13000km kwa speed ya 7.8km kwa sekunde(Mach 23).
Mpaka sasa Marekani ina jumla ya makombora haya zaidi ya 450 yakitarajiwa kupunguzwa mpaka 400 chini ya mkataba wa START.
Kombora hili linatarajiwa kustaafishwa mwaka 2030 huku nafasi yake ikichukuliwa na kombora jingine ambapo kampuni mbalimbali za Marekani kama vile Boeing, Lockeed Martin na Northrop Grumman zinatarajia kushindana katika utengenezaji wa kombora hilo jipya chini ya mpango wa Ground Based Strategic Deterrent next generation nuclear ICBM.
Kombora hilo jipya linatarajiwa kuanza kutengenezwa kuanzia 2020 huku ikitarajiwa kua na teknolojia ya juu ya kukwepa ulinzi wa adui pia lenye nguvu kubwa kuliko la hivi sasa.Mpango huo unatarajia kugharimu jumla ya dola bilioni 86.
UPDATES:
Jaribio limefanyika kwa mafanikio makubwa,kwa mujibu wa jeshi la Marekani.
Kombora lilirushwa toka kambi ya jeshi la anga ya Vandenberg mjini California na kutua karibu na Kwajalein Atoll kwenye visiwa vya Marshall.
Wamesema kwamba kombora hilo liliruka umbali wa zaidi ya maili 4000(kama 7500+km hivi km sikosei).