memael
Senior Member
- Sep 28, 2018
- 104
- 166
HABARI
21.10.2018 | 15:00
Ujerumani yakasirishwa na uamuzi wa Trump wa kujiondoa kwenye mkataba wa nyuklia
Ujerumani imekasirishwa na tamko la rais wa Marekani Donald Trump kwamba anataka kujiondoa kwenye mkataba muhimu na Urusi juu ya kudhibiti silaha za nyuklia. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Niels Annen amesema kwenye mtandao wa twitter kuwa uamuzi wa rais Trump utaleta maafa makubwa. Vyama vya upinzani nchini Ujerumani pia vimetahadharisha kwamba uamuzi huo unaongeza hatari ya kuzuka vita vya nyuklia. naye rais wa zamani wa Urusi Mikhail Gorbachev amemshutumu Trump kwa kutokuwa na busara katika suala hilo. Mkataba huo wa kudhibiti umiliki na uundaji wa makombora ya masafa kati ya kilometa 500 na 5500 ulitiwa saini mnamo mwaka 1987 kati ya Marekani na Umoja wa Kisoviet. Urusi imesema Marekani itakuwa inafanya kosa kubwa iwapo itajiondoa kwenye mkataba huo