kilele pori
JF-Expert Member
- Aug 6, 2013
- 232
- 30
Habarini wana jamvi!! Mimi kwa mda sasa nashindwa kuwaelewa Bodi ya mikopo ya Elimu (HESLB) kwa upande wa Loans repayment kwa wanufaika wote. Moja hii mikopo ina riba au haina, pili inakuaje mtu unapoangalia deni lako (outstanding loan) linakua linatofautiana Mara kwa mara mfano Mimi mwaka jana mwanzoni nliangalia lilikua around 7M Mwaka huu limeongezeka karibia 3M Na mwisho inakuaje watu mmesoma course moja mwaka mmoja Na means test (kwa wakati wetu) sawa lakini mnatofautiana kwenye outstanding loans??
Naomba michango yenu kusaidia manake kulipa deni Ni Wajibu wetu kwa ajili ya ustawi wa nchi ila panaanza Na vikwazo vya ajabu Na vya kukura tena ukizingatia boom lenyewe lilikua linapatikana kwa manati bila migomo Na kelele haliingii kwenye account.
Karibuni,
KILELE PORI.
kwanza haina riba. mbili kiwango kila mtu anakatwa kinategemea na mshahara wake. tatu ulitakiwa uwe na barua inayoonyesha deni lako halisi mwanzoni. nne yawezekana uliangalia vibaya deni lako. hakikisha unapewa barua ya deni lako.
Dawa ya deni ni kulipa, mambo ya "bila kunji pesa haiji" ule ulikuwa utoto!
Mbona mshahara ukichelewa, hakuna kunji?
Wewe ulisainije mkataba wa kukopa bila kusoma masharti yake? Kimsingi mambo yote yapo kwenye ule mkataba uliojaza wakti unaomba bum ukapeleka kwa m/kiti na katibu wa mtaa wakaidhinisha. Mie niliona waliokuwa wanaomba mwaka juzi fomu ilikuwa imeandikwa "riba ni 6% kwa ajili ya kulinda thamani ya hiyo pesa"
1. Najivunia-daiwi nimelipa zote,huu ndio uzalendo rudisha mapema wengine wakopeshwe.
2. Deni Lina penalty ukichelewa kulipa....Kama hiyo ndio unaita riba!
Kuchelewa una maanisha mda gani Na iyo penalty Ni % ngapii?