Shamkware
JF-Expert Member
- Nov 25, 2013
- 1,750
- 2,279
Habari za leo wapendwa wa jukwaa pendwa kabisa,
Heri ya mwaka mpya kwenu wakuu! Hongereni kwa kufika mwaka 2016 salama, kama umefika na vikwazo au matatizo kama mimi jipe moyo.
Hizi ni salamu za shukrani nyingi kwenu wanajamii kama mnakumbuka siku chache zilizopita nilileta maada nikiomba kushea nanyi yaliyokuwa yakinisibu, kiukweli kwa dhati kabisa nawashukuruni nyote mlio nishauri, mlio nipa pole, na hata mlio nikejeri hakika nimejifunza mengi kikubwa nasema asanteni.
Kilichotokea nyuma ya pazia baada ya ushauri wenu mwingi nilipata connection nyingi saaana za wataalamu nimejitahidi kwenda na mke wangu kwa wataalamu hao wa mahusiano na ndoa kwa mazungumzo na ushauri.
Nilishauriwa japo kufanya tofauti nipate likizo kidogo niondoke nae pahala tofauti na nyumbani alipozoea nikaona jambo la msingi. Nilichagua kwenda kutembea nae Zanzibar tutoke Dsm nikafanya booking ya Chumba na kukata ticket za ndege go and return
Cha ajabu huyu mwanamke amekataa kusafiri kwenda huko! Tumevurugana sana. Juzi nikaamua kumpeleka kwao japo akapumzike aniache peke yangu kwa mda amekataa! "Nimeamua kutoa Talaka tatu jana" hakuna namna nyingine potelea kote wacha tugawane kilichopo ntaanza upya mtoto wa kiume...."ama kweli sikio la kufa halisikii dawa"
"NI HAYO YARIYO JIRI ASANTENI"