Marangu Coach Arusha-Dar Poor Customer Service

Richie the1

New Member
Joined
Aug 25, 2014
Posts
3
Reaction score
6
Hawa jamaa walichotufanyia leo tarehe 28 Nov 2019... gari ya kwanza kutoka arusha sio cha kufanya gari za kisasa.

Yaani tumekuja na gari tukiwa tunaelekea Dar ikaharibika Msata (hilo ni jambo la kawaida) sasa namna walivyo handle the situation ndio tatizo linapoanza wametufaulisha kwenye coaster mizigo wakaweka kwenye gari ya pili iliyokua nyuma yetu na hii coaster kumbe tunajilipia na isitoshe inaishia makumbusho huku mizigo yetu tukitakiwa kwenda kuichukua Shekilango.

Nauli ya Dar tumetoa 33k nauli ya Msata-Makumbusho 5k, majibu yao kutoka kwenye ofisi zao zote Dar, Moshi na Arusha ni mabovu na wanakukatia simu mteja.

Kwa hali hii mimi binafsi kupanda hii gari pale nitakapo kosa kabisa gari ya kupanda jambo ambalo ni gumu sana kwa karne hii option zimekua nyingi biashara huria huwezi ku treat mteja kipuuzi kiasi hiki na ukategemea kukutangaza vizuri kurecommend wengine.

Mimi nimepanda kwa recommendation ya mtu ambaye hajawahi panda alisikia tuu kwa mtu, na yeye baada ya kusikia hivi hana mpango wa kupanda tena sasa hapo tuu ni wateja watatu.

Wabadilike laa sivyo wateja tunahitaji huduma siku hizi sio enzi za Mwalimu hizi.
 
Richie the1,
Kwanza ungetulia kisha ungetueleza hali halisi na nini kilitokea, basi liliharibika au lilikatisha safari na kurudi Arusha? Na mizigo ni ipi, ya kisamvu cha mlima Meru? Ndiyo sababu waliogopa kuja nanyi mpaka Dar? Mlishushwa kwa nguvu au mliteremka wenyewe kwa usalama wa kisamvu chenu? Aisee mbona maswali ni mengi mno na ninahofia hautaweza kuyajibu.
 
Kisamvu cha kisimiri kule juu Hatar sna
 
Kwanza ungetulia kisha ungetueleza hali halisi na nini kilitokea, basi liliharibika au lilikatisha safari na kurudi Arusha? Na mizigo ni ipi, ya kisamvu cha mlima Meru? Ndiyo sababu waliogopa kuja nanyi mpaka Dar? Mlishushwa kwa nguvu au mliteremka wenyewe kwa usalama wa kisamvu chenu? Aisee mbona maswali ni mengi mno na ninahofia hautaweza kuyajibu.
hivi moshi kumbe kuna kisamvu mkuu nilikuwa sijui alafu hawa ndugu zetu wanakula kumbe kisamvu
 
Halitoki Moshi, basi linaanzia safari Arusha, Marangu Coach ni jina tu wala haliijui njia ya Marangu. Huko Arusha mzigo wa kisamvu cha mlima Meru kina bei nzuri sana wanakipakia njiani na kushusha hivyohivyo.
 
Richie the1,
Delux train za abiria dar to Moshi soon zinaanza, huo ndio utakuwa dawa ya kudumu na bei nafuu na iko faster na huduma nzuri ndani meanzo mwisho. Kama hawana customer care next month wakaanze kutafuta kazi nyingine za kufanya au biashara zingine kwa suluhisho la kudumu JPM ameshaliona na kulifanyia kazi, rupate deluxe yetu.
 
Hizo ni stori mabasi watu watapanda na biashara itaendelea,treni ipo miaka ya kwenda kigoma na mwanza mabasi yapo na yanajaa kila siku mwz to dar
 
Endelea kwenda bank kuchukua mikopo ya kununua mabasi Kama next year hutaokota makopo mjini
 
Mimi nilipenda policy yao ya ukifikisha tiketi nane unapewa moja bure
 
Delux train za abiria dar to Moshi soon zinaanza, huo ndio utakuwa dawa ya kudumu na bei nafuu na iko faster na huduma nzuri ndani meanzo mwisho. Kama hawana customer care next month wakaanze kutafuta kazi nyingine za kufanya au biashara zingine kwa suluhisho la kudumu JPM ameshaliona na kulifanyia kazi, rupate deluxe yetu.
Hivi hilo Dubwana linatumia siku ngapi kufika moshi,kwani nimeanza kulifikiria Decemba hii. Nijulishe mkuu usikute litakaa njiani siku mbili nikala poketi money yote.
 
Hizo ni stori mabasi watu watapanda na biashara itaendelea,treni ipo miaka ya kwenda kigoma na mwanza mabasi yapo na yanajaa kila siku mwz to dar
trip ya kutumia masaa mawili kwa basi treni itatumia masaa nane, so mtoa mada kwenye hili akae kimya.
 
Kuna tatizo ninaliliona akilini kwangu.waliozaliwa kuanza mwaka 1973 Hadi Sasa hawajawahi kupanda train ya kuja kaskazini kwa Tanzania, hawajui inapita wapi na hawajui raha ya train lands Kama wamekwenda Kanda ya Kati kwa train au nje ya nchi.vinginevyo watatoa kila neno kuhusu train tunayozungumzia.hata wakataji wa ticket za mabasi kuelekea kaskazini au dar hawajawahi kupanda train.hili ni tatizo kubwa na ni vugumu muelewa tunachoongea.ushauri , wasubiri Xmas ya mwaka huu dar to Moshi wataisoma namba.
 
Kuna basi moja la marangu lina mtoto mmoja mkali sana. Ananifanya nilitumie sana gari lao bila kujielewa.
 
Tatizo watu wa Arusha mnaishi kwa mazoea sana, magari kwa sasa yapo kibao, ila watu wameng'ang'ania Marangu sijui Kilimanjaro.... Nilisafiri na BM jamaa wako vizuri sana, ata wale wanaitwa Extra Luxury. Hao wengine wanajivunia ukongwe wao.
 
Back
Top Bottom