Marais wastaafu Tanzania huwapa wakati mgumu warithi wao.

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,252
2,000
Marais wa Tanzania wanaostaafu kuanzia kwa Mkapa hadi Kikwete wamempa na wanaendelea kumpa wakati mgumu sana Rais Magufuli, hii ni kwa sababu, kila eneo ambalo Rais Magufuli anagusa, hakosekani mmojawapo na hasa hasa JAKAYA KIKWETE, sijui alienda ikulu kufanya nini?

IPTL anatajwa sana JAKAYA KIKWETE na familia yake kupitia SIMBA TRUST, Makinikia anatajwa sana huyu mtu, huko Bandarini alitajwa sana huyu mtu, bado Kusafirisha wanyama hai nasikia huko napo anatajwa sana, sasa najiuliza, huko Ikulu alienda kufanya nini?

Kwa kweli wanampa wakati mgumu sana huyu Mh. JPM maana wakati mwingine wanaweza kuhisi kuwa JPM anawatafuta kumbe hakuna!
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,426
2,000
Na umeshawahi kujiuliza jinsi huyo JPM atakavyompa wakati mgumu atakayekuja baada yake kama atatokea CCM?

Hadi leo ni wenyewe tu ndio wanafahamu mchakato wa ununuzi wa Bombardiers umefanyika fanyika vipi

Hadi leo ni wenyewe tu ndio wanafahamu mchakato wa ununuzi wa Boeing umefanyika fanyika vipi

Hapo hata miaka 2 bado haijaisha!!!

Sijazungumzia vi-scandle vidogo vidogo kama vya kujenga Internatonal Airport Chato!!!

Sijazungumzia vi-scandle vidogo vidogo kama vya kujenga mabohari ya MSD Chato na Ruangwa wakati kuna kanda zingine bado hawana bohari za MSD!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom