J.K. NYERERE
Huyu Mzee pamoja na sifa kedekede anazomwagiwa hivi Sasa, safari yake haikuwa rahisi. Alipewa majina ya HAAMBILIKI na MCHONGAMENO. Alichukua hatua kadhaa Ili kukabiliana na upinzani dhidi ya malengo mahususi ya kipindi kile, ya kujenga siasa ya ujamaa pamoja na umoja wa kitaifa, ikiwemo kuondoa mfumo wa chama kimoja, kutoweka mfuko Haki za binadamu katika Katiba, Kianzisha vijiji vya ujamaa n.k
Alipingwa kisiri Siri na hata kwa uwazi na wazito ndani ya Serikali yake, the Kambonas, The Mteis, The Tumtemekes, The Hans Popes etc
Maadui wa Kibepari ndio usiseme. Wengi watakubali hata kuunda Muungano na Zanzibar kwa jinsi ulivyo kwa kipindi kile ulichochewa sana na sababu za kiusalama
Akiendelea kujenga Nchi mara Iddi Amini naye akaibuka. Tanzania ikaenda vitani kwa miaka 2 na ushee
Mwalimu Aliponea chupuchupu kupinduliwa MARA TATU kati ya mwaka 1963 Hadi 1983.
Mwaka 1984 akaona hata hivyo imetosha kwa upande wake, AKAN'GATUKA
MZEE MWINYI
Huyu alimpokea Mwalimu, alianza vizuri kwa kufungua Nchi, maana Nchi Ilikuwa dhofuli Hali kiuchumi, kutokana na vita na haswa siasa za kimataifa.
Kipindi cha huyu Mzee watanzania walishika fedha sana. Enzi hiyo Kuna noti za Blue. Akasema sitaki tabu, Kila Mtu afanye anavyotaka ila heshimu Sheria, RUKSAA..
Mara mfumo wa chama kimoja ukabadilika ukaja vyama vingi, Sasa freedom of expression and joining political party of your choice vikatamalaki. Pamoja na furaha hiyo, Watu wakachoka, akalaumiwa anauza Nchi, anatawaliwa na Mkewe, Watu Wana pesa kuliko Serikali, Nchi inapewa waarabu, Wataanganyika wanataka Serikali Yao, Muungano ukajadiliwa Ili uvujwe, Mwinyi akazidiwa ikabidi Mwalimu aingilie kati, Upinzani wa Lyatonga Mrema ukawasha moto, Hadi watu wakaamini CCM ndio basi tena. Zanzibar ikataka kujiunga OIC iwe mvua iwe jua N.k
Hatimaye mda ukafika salama akampisha mwingine
MZEE MKAPA.
Huyu akaanza na gia ya UWAZI NA UKWELI. Ukisikiliza hotuba zake unashiba matumaini. Uwazi Nchi Haina fedha, Ukweli Serikali wameshindwa kusimamia uchumi, akataka private sector iimarishwe.
Wazungu wakampenda, msaada ikaongezwa na madeni yakafutwa. Thubutuuu kumbe ndani yake Kuna wanamtandao, kumbe Zanzibar kuna moto, Wakimbizi wa kipemba wakazuka. Siasa za ngunguri na ngagari zikashika kasi.
Akaanza kuitwa mnywa Damu, anauza Mali za Umma, Analeta Ukapa kwa Nchi kama lilivyo Jina lake, akapigwa vijembe Hadi vya familia yake nakadhalika.
Mda ukafika akampisha mwingine
MZEE KIKWETE
Huyu aliingia na Ari mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya. Kafanya mengi haswa kwa miundo mbinu, utawala Bora, kuimarisha Demokrasia, kujenga diplomasia ya kimataifa na kuvuta wawekezaji wengi na mengine mengi.
Lakini Ghafla kibao kikabadilika, zikaja hoja za RUCHMOND, MERIMETA, Waziri wake Mkuu akajiuzulu, hata badae mawaziri wake wengine wakajiuzulu, enzi za Bunge la Kasi na viwango, akaanza kuiitwa dhaifu, ana chekacheka, anaendesha Nchi kifamilia, na Vasco da gama na mengine mengi. Watu wakaomba ni heri wapate Raisi dikteta kuliko huyu, na mengine mengi
Wakati ukafika salama akampisha mwingine
MZEE MAGUFULI
Huyu aliingia na hapa kazi tu. Na kweli mwanzoni alitaka wasiofanya kazi wakamatwe, akataka Nchi ya viwanda, akaanzisha mahakama ya mafisadi, Kwa njia zinakobalika na hata zisizokubalika, akapambana Shirika la ndege likafufuka, ndoto ya bwawa la Nyerere ikaamka, treni za mwendo Kasi hizo, akaona Ili afanikiwe zaidi apige ban shughuli za siasa, maana kiukweli zinachelewesha mambo.
Badae kibao kikageuka, anakandamiza Haki za binadamu, watu wanaompinga wanapotea na kuuwawa, anakandamiza wafanyakazi, ni mbabe, Matendo ya watu wasijulikana, nakadhalika.
Naye akaondoka kwa kifo makamu wake akaendelea kwa mujibu wa Katiba.
MAMA SAMIA
Huyu akaona aje na KAZI IENDELEE. Yaani kazi zote za awamu zilizopita aendeleze na kuzikamilisha. Akaja na kauli mbiu ya 4 R Ili kuleta umoja na maelewano ya kisiasa nchini. Kafanya mengi kuanzia na kuendeleza na kukamilisha kazi za mtangulizi wake, huduma za kijamii, kubuni njia za kufungua na kukuza uchumi nakadhalika.
Lakini huyu naye yalianza hata kabla hajakalia kiti vizuri, uanamke wake haukukubalika kwa Vigogo wa juu Serikalini kwa sababu zao. Nadhani kama sio CDF Mobeyo kuingia kwake madarakani kungekuwa kugumu sana. Wengi wakatabiri hata hivyo hatafika mbali, yatamshinda tu.
Pamoja hayo, shutma zikaanza anauza Nchi kwa waarabu, ana upendeleo wa ki Zanzibari, Ni mwanamke hivyo hawezi kulifikisha popote Taifa hili, anahusika na utekaji na watu kupotea, Nakadhalika.
NDIO UONGOZI
KAZI IENDELEE