Marais wa Marekani waliokumbana na mambo ya ajabu

Marais wa Marekani waliokumbana na mambo ya ajabu

ShyaRuwa

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
8,453
Reaction score
15,380
1.GROVER CLEVELAND: Kabla ya kuwa Rais, alikuwa mnyongaji wa wahukumiwa wa hukumu ya kifo.Ni rais aliyeongoza kwa mihula miwili isiyofuatana 1885-1889 na 1893-1897.

2.HARRY S TRUMAN: 'S' iliyopo kwenye jina lake siyo kifupi cha jina, hivyo haimaanishi chochote.

3.JOHN F.KENNEDY: Ndiye Rais wa kwanza wa Marekani kuzaliwa karne ya 20, ndiye Rais pekee wa Marekani mkatoliki na ndiye Rais wa US mwenye rekodi ya kuwa na michepuko mingi zaidi.

4.Marais watatu wa Marekani; John Adams, Thomas Jefferson, na James Monroe walifariki tarehe 4 July.Ni rais mmoja tu, Calvin Coolidge aliyezaliwa tarehe 4 July.Tarehe hiyo hiyo ni tarehe ya uhuru wa Marekani.

5.JAMES GARFIELD: Huyu alikuwa na uwezo wa kuandika kwa mikono yote miwili, kwa lugha mbili tofauti[Kilatini na Kigiriki] na kwa wakati mmoja.

6. Mauaji ya marais watatu wa Marekani; ABRAHAM LINCOLN, JAMES GARFIELD, na WILLIAM MCKINLEY yalishuhudiwa na mtoto wa kwanza wa ABRAHAM LINCOLN aliyeitwa ROBERT LINCOLN.

7.WARREN G.HARDING: Huyu alikuwa mcheza kamari wa kupindukia.Aliwahi ku-bet karibu vitu vyote vya thamani vya White House na kupoteza.

8.THEODORE ROOSEVELT: Wakati akiwa kwenye kampeni za kuwania urais kwa mara ya pili alipigwa risasi, lakini aliendelea kuhutubia hadi mwisho wa mkutano wa kampeni ili hali risasi ipo mwilini.

9.ANDREW JOHNSON: Huyu alikuwa fundi cherehani wa kwanza kuwa Rais.Suti alizovaa alizishona mwenyewe.

10. Marais sita waliitwa JAMES. Nao ni Madison, Monroe, Polk, Buchanan, Garfield, na Carter.

11.RICHARD NIXON: Alikuwa Rais wa kwanza kutembelea majimbo yote 50 ya US na ndiye Rais wa kwanza wa Marekani kufika/kutembelea China.

12.JAMES BUCHANAN: Yeye alikuwa Rais Bachelor, hakuwa na Mke, kwa hiyo kwenye utawala wake nchi haikuwa na First lady.

13. JOHN TYLER: Ndiye Rais wa Marekani aliyekuwa na watoto wengi zaidi.Alikuwa na watoto nane kwa mke wa kwanza na watoto saba kwa mke wa pili.Ndiye Rais pekee wa Marekani kuoa akiwa ofisini[alipooa kwa mara ya pili].

14.ZACHARY TAYLOR: Huyu alikuwa Rais wa Marekani kwa muda usiozidi mwaka mmoja na nusu.Alifariki sababu ya ugonjwa wa kipindupindu.

15.GEORGE HERBERT WALKER BUSH: Ndiye Rais pekee wa Marekani aliyekuwa na majina manne.Alipoitembelea Japani Jan 8 1992, wakiwa kwenye chakula cha jioni alimtapikia aliyekuwa waziri mkuu wa Japani KIICHI MIYAZAWA na kupoteza fahamu.Tukio la BUSH Sr kutapika liliwapa wajapani msamiati mpya kwenye lugha yao ''BUSHU-SURU'' ukiwa na maana ya kutapika hadharani.

16.GEORGE WASHINGTON: Baada ya kuwa rais hakuwa na pesa za kugharamia safari ya kuapishwa kwake.Hivyo alimkopa jirani yake dola mia sita ili aweze kuhudhuria kuapishwa kwake pamoja na kujilipia madeni.
 
Hiyo namba mbili sijakuelewa hapo,kwani ukiwa na s isiyoeleweka kwenye jina lako ni ishara ya kukumbana na mambo ya ajabu?
 
Ninayempenda ni James Polk...aliahidi akichaguliwa hatogombea uraisi kwa muhula wa pili maana atafanya yote aliyopanga kuyafanya (na kuahidi kuyafanya) ndani ya muhula mmoja tu.


..na alitimiza ahadi yake!!!
 
Back
Top Bottom