Taifa la Marekani mpaka sasa 2014 limekuwa na jumla ya marais 44 tangu kupata uhuru wake mwaka 1732. Mtandao wa 24/7 Wall St hivi karibuni ulitoa orodha ya marais hao na utajiri wao. Orodha hiyo imeonyesha tofauti kubwa ya utajiri wa marais hao, wapo ambao walikuwa ni matajiri sana, kama George Washington anayekadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya dola nusu bilioni kwa fedha ya leo. Lakini vilevile wapo marais ambao mpaka mwisho wa maisha yao walikuwa tayari wameshafilisika. Lakini jambo moja ni dhahiri, inalipa kuwa rais wa taifa kubwa kama Marekani.
Rais Bill Clinton aliyeongoza taifa hilo tangu mwaka 1993 had 2001 ni miongoni mwa marais kumi matajiri zaidi wa Marekani, na kati ya hao Bill Clinton ni peke yake aliye hai hivi sasa. Rais wa sasa wa Marekani, Barack Obama sio miongoni mwa marais matajiri sana. Yeye hupokea mshahara wa dola 400,000 kwa mwaka na anakadiriwa kuna na utajiri unaofikia dola milioni 7.5. Sehemu kubwa ya utajiri huo inatokana na mauzo ya vitabu vyake.
Orodha ya Marais Kumi Matajiri Zaidi Marekani
10. John Fitzgerald Kennedy
Rais wa 35 wa Marekani tangu 1961 hadi 1963
Thamani halisi ya utajiri wake: Dola bilioni moja
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]
John Fitzgerald Kennedy[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Kennedy alizaliwa katika familia tajiri, baba yake akiwa ni miongoni mwa watu matajiri zaidi Marekani. Sehemu kubwa ya mapato na utajiri wa Kennedy unatokana na muamana aliokuwa akishirikiana na ndugu zake.
9. William (Bill) Jefferson Clinton
Rais wa 42 wa Marekani tangu 1993 hadi 2001
Thamani halisi ya utajiri wake: Dola milioni 55
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Bill na Hilary Clinton[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Tofauti na marais wengine wa Marekani, Clinton hakurithi chochote kutoka kwa wazazi wake na wakati wote wa miaka yake zaidi kidogo ya ishirini ya utumishi wa umma aliweza tu kujiwekea akiba kidogo. Baada ya kumaliza muda wake wa urais, Bill Clinton ameweza kujipatia utajiri kwa kupitia uandishi wa vitabu na kutoa mihadhara. Mathalani mwaka 2005 Clintoni alilipwa kiasi cha dola milioni 15 kama malipo ya awali ya kitabu chake, "My Life". Mwaka 2011 Clinton alilipwa dola 750,000 kwa kutoa mhadhara huko Hong Kong kwa ajili ya kampuni ya Ericsson. Mama Clinton pia amekuwa akichangia pato la familia hiyo kwa njia ya uandishi wa vitabu na mihadhara ambapo inakadiriwa kuwa hulipwa kiasi cha dola 200, 000 kwa kila mhadhara anaotoa.
8. Franklin Delano Roosevelt
Rais wa 32 wa Marekani tangu 1933 hadi 1945
Thamani halisi ya utajiri wake: Dola milioni 60
Utajiri mkubwa wa Roosevelt ulitokana na urithi na ndoa. Roosevelt alimilki shamba la ekari 800 na majumba huko Georgia, Maine na New York.
7. Herbert Clark Hoover
Rais wa 31 wa Marekani tangu 1929 hadi 1933
Thamani halisi ya utajiri wake
: Dola milioni 75
Herbet Clack Hoover alikuwa mtoto yatima aliyelelewa na mjomba wake aliyekuwa daktari. Hoover alipata utajiri mkubwa akiwa kama mtendaji mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini, nafasi aliyoishikilia kwa miaka 17 akilipwa mshahara mnono. Wakati alipokuwa rais, Hoover aliutoa mshahara wake kwa shirika la upendo.
6. Lyndon Baines Johnson
Rais wa 36 wa Marekani tangu 1963 hadi 1969
Thamani halisi ya utajiri wake: Dola milioni 98
Baba yake Johnson alipoteza fedha yote ya familia wakati Lyndon akiwa bado kijana mdogo. Licha ya hayo, Lyndon aliweza kujikusanyia utajiri hata akaweza kumiliki ekari 1,500 huko Blanco. Ndani ya shamba hilo pia ilikuwemo nyumba yake iliyojulikna pia kama "the Texas White House". Lyndon pamoja na mkewe pia walimiliki kituo cha redio na television huko Austin, Texas na pia walikuwa na mali nyingine kama mifugo na ndege za kukodisha.
5. James Madison
Rais wa 4 wa Marekani tangu 1809 hadi 1817
Thamani halisi ya utajiri wake: Dola milioni 101
Madison ndiye aliyekuwa mmiliki mkubwa wa ardhi kupita wote huko Orange, Virginia. Ardhi aliyokuwa anamiliki ilipata ukubwa wa ekari 5,000. Madison alipata utajiri huu wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na pia alipokuwa rais. Hata hivyo, Madison alipoteza utajiri wake wakati alipokaribia mwisho wa maisha yake kwa sababu ya matatizo ya kifedha katika shamba lake.
4. Andrew Jackson
Rais wa 7 wa Marekani tangu 1829 hadi 1837
Thamani halisi ya utajiri wake: Dola milioni 119
Wakati alitambuliwa kama mtu anayewajali watu wa kiwango cha kati cha maisha, Jackson alijikusanyia utajiri mwingi kimya kimya hata kuwa rais tajiri kupita wote katika miaka ile ya 1800. Alimiliki shamba lenye ukubwa wa ekari 1,050 na alikuwa na watumwa wapatao 300 wakati wa maisha yake. Hata hivyo, baadae Jackson aliingia katika madeni makubwa.
3. Theodore Roosevelt
Rais wa 26 wa Marekani tangu 1901 hadi 1909
Thamani halisi ya utajiri wake: Dola milioni 125
Theodore Roosevelt alizaliwa katika familia maarufu na tajiri na alipokea urithi mnono. Hata hivyo, Roosevelt alipoteza utajiri wake wakati alipojaribu kuwekeza katika ufugaji mkubwa hata akalazimika kuishi kwa kufanya kazi ya uandishi. Roosevelt alitumia sehemu kubwa ya maisha yake katika utumishi wa umma na aliweza kumiliki shamba lenye ukubwa wa ekari 235 huko Long Island.
2. Thomas Jefferson
Rais wa 3 wa Marekani tangu 1801 hadi 1809
Thamani halisi ya utajiri wake: Dola milioni 212
Jefferson alirithi kiasi cha ekari 3,000 na watumwa wengi kutoka kwa baba yake. Thomas Jefferson pia aliweza kujipatia utajiri akifanya kazi katika nyadhifa mbalimbali za kisiasa kabla ya kuwa rais wa Marekani. Hata hivyo wakati anakaribia mwisho wake, Jefferson alijikuta katika madeni makubwa.
1. George Washington
Rais wa kwanza wa Marekani tangu 1789 hadi 1797
Thamani halisi ya utajiri wake: Dola Milioni 525
George Washington alimiki shamba lenye ukubwa wa ekari 8,000 huko Virginia lililokuwa likiendeshwa na watumwa wapatao 300. Pia, mke wake, Martha, alirithi mali nyingi kutoka kwa baba yake. Akiwa rais, George Washington alilipwa zaidi kuliko marais waliomfuata. Mwaka 1789 mshahara wake ulikuwa asilimia 2 ya bajeti yote ya Marekani.