Marafiki wa mahakama; rufaa ya mgombea binafsi

pangamawe

Member
Jan 18, 2009
8
0
Watanzania kwa ujumla wetu tunasubiri kwa hamu kubwa hukumu ya rufaa iliyokatwa na serikali kuhusu mgombea binafsi. Nampongeza sana mhe jaji mkuu Augustino Ramadhani kwa namna alivyoshtukia janja ya CCM kutaka kupoteza muda ili kesi ichelewe kusikilizwa hivyo suala la mgombea binafsi kutofikia uamuzi mapema. Ukisikia tambo zinazotolewa na viongozi wa CCM juu ya jinsi chama chao "kinavyokubalika" unapatwa na mshangao ni kwanini chama hicho pamoja na "kukubalika kwake huko" kiogope mgombea binafsi kiasi hicho. Wenye akili wanajua ukweli wa mambo kuwa chama hicho hivi sasa kinakubalika miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa, viongozi na familia zao tu kwa jinsi kinavyoifisadi nchi yetu.

Nimeanza kwa kumpongeza jaji mkuu kwa hatua aliyochukua kuona kwamba kesi hiyo inamalizika mapema na haki itendeke, napongeza sana wazo la kualikwa mahakamani marafiki wa mahakama katika azma nzima ya kuhakikisha haki inatendeka. Tatizo langu ni katika composition ya marafiki hao wa mahakama walioalikwa. Kumualika DPP wa Zanzibar na Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi NEC mtu yeyote bila kuhitaji kuwa na "utaalamu" wa utabiri alionao Shekh Yahya Husein angeweza kubashiri maoni ya watu hao wawili yangeegemea wapi. Ni dhahiri watu hao wawili walilazimika kuunga mkono msimamo wa mwajiri wao ili wasipoteze vibarua vyao, lingekuwa jambo la ajabu sana kama wawili hao wangeamua kuweka ukereketwa wao pembeni na kutetea maslahi ya watanzania walio wengi. Hivyo mheshimiwa jaji mkuu uliteleza katika kuteua wawili hawa. Kuhusu maprofesa Jwani Mwaikusa na Palamagamba Kabudi watanzania wengi walitegemea hawa wangeishauri mahakama kitaalamu kulingana na weredi walio nao katika fani ya sheria na si kuegemea upande wowote.

Profesa Mwaikusa na Prof Kabudi walitofautiana juu ya uwezo wa mahakama kusikiliza kesi hiyo, Prof Kabudi alidai mahakama hiyo haina madaraka wakati Prof Mwaikusa alisema mahakama inayo madaraka ya kusikiliza kesi hiyo. Prof Palamagamba Kabudi kama ilivyo kwa DPP wa Zanzibar na Mkurugenzi wa NEC hakuwa na chaguo zaidi ya kulinda maslahi ya "mwajiri wake". Prof Kabudi ni mwerewa mzuri sana wa sheria, nikiwa kama mwanasheria naukubali weredi wa prof Kabudi katika sheria na uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja na kujieleza. Wengi hamfahamu hili na hata mhe jaji mkuu hafahamu kuwa prof Kabudi ni afisa usalama wa taifa ambaye alihitimu mafunzo yake katika chuo cha usalama wa taifa MALINDI mwishoni mwa miaka ya sabini. Hivyo pamoja na kufanya kazi muda mrefu chuo kikuu cha Dar es Salaam bado anajukumu la kulinda na kupigania maslahi ya serikali kila inapotokea fursa kama ilivyotokea hii ya kualikwa kama rafiki wa mahakama.
 
Taarifa yako juu ya Kabudi imenifanya nielewe sababu za huyu mwanazuoni. Hapo mwanzo nilifikiri kuwa yuko njiani kumfuata mwenzake Mwakyembe kupata ridhaa ya CCM lakini kumbe hali ni tete zaidi. Ama hili la Mkurugenzi wa Zanzibar , kosa limefanyika pale. Anaelalamika ni Serikali halafu tunamchukuwa Afisa wa Serikali tupate mawanzo yake. Tukubali Jaji Mkuu alikosea kumkaribisha Mkurugenzi wa mashtaka wa Zanzibar.
 
jee,mlitaka nani aitwe kama rafiki wa mahakama?ule ni ushauri tu ambao si binding kwa mahakama. Mahakama ndiyo yenye uamuzi a mwisho ktk suala hilo. Tusubiri tuone...
 
Back
Top Bottom