Marafiki siku njema

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,440
Reaction score
38,437
Awali ya yote, niwatakie 14 Feb njema wana Jamii forums.

Huitaji kamusi yoyote ile kujua maana ya dhana nzima ya urafiki, na washiriki wake-marafiki.Urafiki hujengwa kwa njia nyingi sana, msingi mkubwa ukiwa ni ule wa "ndege wafananao, huruka pamoja"

Mara nyingi urafiki hujengwa kwa bahati, sina uhakika km ni bahati mbaya ama nzuri.Ila bahati huleta urafiki, marafiki na ndio maana pia, hata kuvunjika kwa urafiki mwingi, hutokea katika hali ya sintofahamu.

Mungu ni mwingi wa maajabu urafiki huweza kuchipua popote pale, iwe penye raha, ama karaha
msibani safarini.

Hata bar, sokoni, harusini shuleni!
N.k.

Naomba kukumbusha nguzo moja muhimu ya urafiki,uwekezaji urafiki uwe urafiki, ni lazima kwa marafiki kuwekeza.Hata zile kauli kuwa,katika marafiki zangu wote, huyu ndie rafiki.Katika watu wakionibeba, marafiki zangu sitawasau, bila ya xx, rafiki yangu huyu, nisingekuwa hapa.

Hizi ni viashirio vya uwekezaji kwenye urafiki.Urafiki mwingi hufa kwa vile wahusika hawakuwa tayari kuwekeza! Wakati mwingine uwekezaji usio sahihi huu urafiki.

Na hapa kuna angalizo marafiki wengi, wanaolalamikia kusalitiwa ktk urafiki, utagundua kosa kubwa katika uwekezaji uliofanywa,hili huleta kilio na maumivu.

Kilio maumivu haviletwi na kuvunjika kwa urafiki ule nyuma ya pazia uwekezaji uliofanyika ndio unaoliza marafiki! Ndio unaoumiza marafiki.

Urafiki umedumu, watu wametumia muda wao fedhwa, maarifa ujuzi. Na rasilimali kadhaa, Hivi ndio huumiza pale usaliti unapojitokeza ukubwa wa uwekezaji ndio ukubwa wa maumivu pindi usaliti utokeapo.

Kama hivo ndivo, hutaki kuumizwa na marafiki, hutaki kulizwa na marafiki! Jitoe katikauwekezaji wa urafiki.Kwa nini ujiumize kwa nini ujilize,lakini pia usisahau, marafiki ni watu muhimu sana, angalizo ni namna gani umewekeza ktk urafiki huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…