Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Zaidi ya nyumba mia tatu katika kitongoji cha Nyabichune ambazo zimejengwa ndani ya eneo la leseni ya uchimbaji wa madini ya kampuni ya ACACIA kupitia mgodi wake wa North Mara wilayani Tarime mkoani Mara, zimebomolewa chini ya ulinzi mkali wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo baada ya wamiliki wake kulipwa fidia kisha kukaidi kuhama katika eneo hilo hatua ambayo imetajwa kusababisha mgodi huo kufikiria kusitisha shughuli zake za uchimbaji.
Akizungumza wakati akitangaza kuvunjwa kwa nyumba hizo, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Bw. Glorious Luoga, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Tarime, amesema hakuna mjadala tena kuhusu jambo hilo kwa sasa kwa vile wananchi hao mbali na kuvamia maeneo ya leseni ya mwekezaji na kuanza kujenga nyumba kwa mtindo wa tegesha, bado serikali iliomba mgodi kulipa fidia ili kunusuru shughuli za uendeshaji wa mgodi kusitishwa, lakini inashangaza kuona baadhi ya watu wakikaidi kuhama huku wakishinikiza kulipwa fidia kubwa kinyume cha sheria.
Naye meneja uendeshaji wa idara ya ardhi katika mgodi huo wa North Mara Bw. Abel Yiga, amesema baada ya amri hiyo ya mkuu wa wilaya, uongozi wa mgodi utalipa wananchi ambao wako tayari kwa kuongeza malipo hayo mara sita na yale yanayotakiwa kama fidia za serikali, huku mmoja wa mwananchi katika eneo hilo akipongeza uamuzi huo wa serikali.