Mara: Ajali yaua 5 na kujeruhi 3 Tarime

Mara: Ajali yaua 5 na kujeruhi 3 Tarime

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,175
Reaction score
64,552
Rorya mara ;

Ajali mbaya sana imetokea rorya kijiji cha mika kitongoji cha bukwe kwa gari aina ya probox yenye namba za usajili t 258 bgb.Kwa maelezo ya shuhuda alienusurika kwenye ajali hiyo bi fides fedrik mkazi wa bunda miaka 29 amesema walikuwa wanatokea busurwa wakienda tarime.

Walisimamiswa na wanaodhaniwa ni askari wa maliasil wakiwa wamevaa magwanda ya askari wa maliasili. Walisimamisha gari walio kuwa wanasafiria lakini dreva alikataa kusimama kwa madai kwamba sio askari .Lakini katika kuwafukuza dereva ambae ndie mmiliki wa gari iliyo pata ajali hakuweza kutii .

Muda huo alikuwa anaendesha akiwa ana zima zima taa kwa sababu ambazo nao walihisi ni kuwakwepa hao askari wa mali asili.Hadi walipo fika bukwe walijikuta wamepata ajali na wenzao watatu 3 kufariki papo hapo na wawili kufia hosptali wakipata huduma .Pia shuhuda mwingine ndugu thomas omware laban amesema yeye pia alisimamishwa na hao watu wakikagua buti za magari kwa maelezo kwamba wanakagua mazao ya samaki .Kwamba walikuwa wanasimamisha kila gari na kuikagua.

Alishuhudia gari hii ikisimamishwa lakini dereva bwana masiaga athumani ambae ni marehemu hakuweza kusimama ndipo hii gari ya hawa maliasili aina ya land cruza yenye mkonga ilianza kufukuzana na gari hiyo hadi bukwe ilipo patia ajali na wao kugeuza gari baada ya kuona hiyo gari imepinduka tena bila kutoa msaada wowote wa kibinadamu wa kuokoa majeruhi na wahanga hao wa ajali,

Nae diwani wa nyamagaro mh masana amesema amesha kutana na hawa watu wakitoza ushuru ambao ni haki ya halimashauri ya rorya na akazuia kwa madai kwamba hawawezi kutoka msoma kuja kutoza ushuru rorya tena ni uporaji . Amesema mh masana. Mh masana amesema kuwa wafanya biashara hawa waliopata ajali wote walikuwa wanatokea kwenye kata yake ya nyamagaro, mwalo wanyang'ome wilayani rorya kwenye ajali hiyo wamefika viongozi wa polis kanda maalu tarime /rorya wakiongozwa na rco maya na ocd wa rorya asp sarige kushugulikia uokoaji wa wahanga wa ajali. Na kuanza kufanya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo, ambapo wamewataka wananchi walio fika kwenye eneo la tukio kuwa watulivu na kuacha polis ifanye uchunguzi wa ajali hiyo.

Habari na thomas nkaina wa kituo cha habari na mawasiliano rorya

=====

Gari ya kubeba abiria wa Samaki kutoka Shirati na kwenda Tarime Leo asubuhi limepata ajali na kuua watu 5 na kujeruhi wengine 3.


Kamanda mkoa wa kipolisi,Tarime na Rorya,Henry Mwaibambe amewaambia waandishi wa habari kwanjia ya simu ya kiganjani kuwa kati yao waliokufa in Dereva wa gari hill,Masiaga huku marehemu wengine majina hayaja julikana.


Mwaimbe ameingeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi baada ya dereva hiyo kusimamishwa na polisi kisha kukaidi na kisha gari kujigonga kwenye tuta(bams).


pia Mwaibambe ameongeza kuwa ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi wakati gari likiwa linatoka Shirati kuelekea Tarime huku likuwa limebeba wafanyabiasgara wa Samaki na Samaki.

Kamanda mwaibambe amekeme tabia ya baadhi ya madereva kuendesha kwa mwendokasi.
FB_IMG_1534302986844.jpg
FB_IMG_1534302968123.jpg
FB_IMG_1534303004228.jpg
 
Pole kwa wahanga

Ila mambo ya kusimamishana usiku sio mazuri, nitajuaje kama ni askari kweli.
 
Mungu awapumzishe Mahali pema peponi... Figaniga wewe ni Police? Maana una habari za Motomoto
 
Hivi vifo vingine ni vya kizembe sana, unazima taa uko speed!? Yote hii sababu ya kutokutii sheria.
 
Back
Top Bottom