Mapya yaibuka bosi UN kutimuliwa nchini Tanzania

Mapya yaibuka bosi UN kutimuliwa nchini Tanzania

Wana JF,
Hii ni Tanzania ya Magufuli ambayo imeshapoteza mwelekeo kwenye jukwaa la Kimataifa. Sera za CCM ya Magufuli ni uchuro na Mataifa yanaiona Tanzania kwa sasa kuwa ni tatizo katika maswala ya Utawala Bora.
Serikali na Magufuli waache kuongoza nchi kiujanjaujanja kwa kuwafanya Watanzania hawana akili. Swala la kufukuzwa kwa huyu Bosi wa UNDP iliyoko chini ya UN(Umoja wa Taifa) liko wazi. Kusema kuwa huyu Mkurugenzi Awa Dabo kafukuzwa kwa kutoelewaana na Wafayakazi wenzake ni porpjo za kihuni.

Ukweli ni kwamba huyu mama ALITAKA KUSIMAMIA MISINGI YA HAKI NA UTAWALA BORA KULINGANA NA MIKATABA YA UN(UMOJA WA MATAIFA) na si vinginevyo. Hivi kuhoji kuhusu ZEC kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar 2015 ni kutoelewana na Wafanyakazi wenzake? Hivi kwanini Wapinzani walikamatwa wakati wa Uchaguzi Mkuu 2015 ni kutoelewana na Wafanyakazi wenzake? Hivi kuhoji juu ya sheria kandamizi ya Media na Mitandao Tanzania ni kutoelewana na wafayakazi??

UNDP na UN wanahaki ya kuihoji Serikali ya Magufuli kwanini inakandamiza Uhuru wa Habari, Uhuru wa Kujieleza na Demokrasia ya Uchaguzi Huru na Haki na kutoa maamuzi kulingana na vile wanaona hali ilivyo. Fedha ya MCC zaidi ya Trillioni 1 zimezuliwa na Marekani na Misaada mingine muhimu ya Wahisani imesitishwa kwasababu za kipuuzi za Jecha wa Jecha kushirikiana na CCM kuvuruga Uchaguzi Mku wa Zanzibar 2015!!!

JPM na CCM mfikie mahali mkubali UDHAIFU wenu na mrekebisha makosa yenu ili nchi isonge mbele. Mkisha sawazisha huu upuuzi wenu misaada itakuja tu. Lakini kama mnaendelea kukomaa na kushupaza shingo MTAENDELEA KUISOMA namba tu. Tanzania siyo Kisiwa lazima ikubaliane na Mikataba ya Kimataifa ambayo nchi imeridhia na si vinginevyo!!
 
Hii sasa inaingia akilini lakini kutuambia kaondolewa kwa sababu alikorofishana na staffs ni uwongo na uzushi mtupu.
 
Wafanyakazi wa un wana miongozo yao ya kazi, ukitenda kinyume na ustaarabu watarejesha walichoshuhudia. Kuwaweka mkononi ni ngumu, wanalipwa vizuri. Hata ajae hatakuwa tofauti. Suruhi ufunge ofisi yao.
 
Kama boss wa UNDP hakuwa akielewana na wafanyakazi wake hilo serikali haliwahusu kwa sababu shirika hilo linaendeshwa na UN, sasa kitendo cha serikali kuingilia mambo ya ndani ya shirika la UN ni kwamba shirika hilo liko chini ya serikali kitu ambacho hakiwezekani.
Ukiwa kwenye nchi ya watu lazima uelewane na raia wa nchi hiyo ukifanya tofauti unafukuzwa 24 hours inaitwa "PI". Mbona wapo wengi tu wameshafukuzwa nchini kwa matatizo kama hayo? Humkumbuki yule mwaarabu alikorofishana na Traffic alifukuzwa nchini within 24 hours. Ni utaratibu wa kimataifa!
 
Tanzania ni nchi huru, ina maamuzi yake kamili kama nchi na kama dola. haipaswi mtu mmoja kujiona ana ndevu kuliko uhalisia uliopo. ajiheshimu
Lini Tz inepata uhuru?Amka wewe kilaza Tz si huru na lazima ifuate maelekezo kutoka kwa bwana.
 
Ukiwa kwenye nchi ya watu lazima uelewane na raia wa nchi hiyo ukifanya tofauti unafukuzwa 24 hours inaitwa "PI". Mbona wapo wengi tu wameshafukuzwa nchini kwa matatizo kama hayo? Humkumbuki yule mwaarabu alikorofishana na Traffic alifukuzwa nchini within 24 hours. Ni utaratibu wa kimataifa!
Umeelewa kilichoandikwa?
 
Uchaguzi hupoteza gharama nyingi Ile ripoti iliyopinga vyama vingi hiko sahihi maana bado hatukujiandaa ndio maana hata baada ya uchaguzi tunafikiria uchaguzi na si maendeleo. Hii inatugharimu mno
 
Nyumbu waliaminishwa na Mange Kimambi eti kisa ni Mahusiano ya Kingono ya Hoyce Temu na Kigogo wa Serikali![emoji12][emoji12][emoji12]
Una maanisha mange aliwasiliana na Nyumbu? Mie nafahamu nyumbu ni wanyama wa polini na huwa hawaongei na mwanadamu isipokuwa wao kwa wao. Sasa mange kimambi alitumia namna gani kuwashawishi nyumbu kuwa sakata la Awa Dabo kufurushwa nchini ni kutokana na hicho ulichosema!? Na lengo la kuwaambia nyumbu je, alitarajia nini kutoka kwao?
 
MYAONAPO HAYO CHANGAMKENI MKAVIINUE VICHWA VYENU MAANA SAA YA KUJA KWAKE MWANA WA ADAM IMEKALIBIA!
 
"Mwenye haki akitawala hata ndege wa angani na wanyama wa kondeni hushangilia pia"
 
Kama bado tunategemea wahisani na huu ndo mwendo kana kwamba tunajitosheleza, sisi ndo tutakao umia...
 
Inaleta picha kwamba Tz ni nchi huru, halafu gazeti la Mtanzania linaonekana lina agenda yake, kama serikali ilikuwa inataka kumuondoa huyo kwa sababu hizo ingemuondoa mapema sana, ni wazi hili gazeti linatumika na ndio gazeti pia baadhi ya international media wanari quote kama source ya habari yao.

safi sana kiongozi kwa summary
 
Tanzania inazidi kutafuta maadui!!! Tutakaoumia ni sisis masikini!!! [emoji20][emoji20][emoji20]

sisi sio masikini bwana. Hali ya upepo duniani kote imebadilika bwana. Tunatakiwa kuwa na uongozi unaijiamni na sio kutegemea hadi mawazo ya nje yaje yatutawale jaman
 
Mange amewadanganya nyumbu wa CHADEMA
Acha uongo. Nenda tena kwenye Instagram account yake, ametoa ushahidi. Fanyia kwanza kazi ushahidi aliotoa kisha rudi hapa utwambie kama umethibitisha ushahidi aliotoa ni wa uongo. Don't patronize us with your lies. Najua hampendi Mange kwa sababu ya yale mambo yenu ya Punda afe mzigo wa tajiri ufike, lakini lazima ukweli usemwe.
 
Inaleta picha kwamba Tz ni nchi huru, halafu gazeti la Mtanzania linaonekana lina agenda yake, kama serikali ilikuwa inataka kumuondoa huyo kwa sababu hizo ingemuondoa mapema sana, ni wazi hili gazeti linatumika na ndio gazeti pia baadhi ya international media wanari quote kama source ya habari yao.

sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom