Mapya ya Dk Mwaka

Mapya ya Dk Mwaka

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
UAMUZI wa kufunga kituo cha yiba mbadala kinachomilikiwa na Dk. Juma Mwaka umetawaliwa na maslahi binafsi imefahamika, anaandika Mwandishi Wetu.

Taarifa kutoka ndani ya wizara hiyo zinasema uamuzi wa kufunga kituo hicho unatokana na shinikizo lenye maslahi binafsi la kiongozi mwandamizi wa wizara hiyo.

Kituo cha tiba mbadala kinachomikiwa na Dk. Mwaka kilifungwa mwezi uliopita kwa amri ya Dk Hamis Kigwangala Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Anayetuhumiwa kumuingiza pabaya Dk. Kigwangala ni mmoja wa madaktari wanaofanya kazi makao makuu ya wizara Jijini Dar es Salaam ambaye kwa sasa yupo masomoni nje ya nchi.

Kwa habari zaidi soma gazeti la MSETO la leo Agosti 11, 2016 pia unaweza kusoma magazeti ya MSETO na MwanaHALISI kupitia mPaper na Sim Gazeti.
 
Gazeti lenu la udaku lishafungiwa kwa miaka mitatu. Udaku udaku, kama lina uhakika si limtaje huyo daktari tumjue.
 
Lisemwalo nalo linaweza likawepo.
Time will tell, just a matter of time... Tutajua mengi tu
 
Mi nikiona story kama hii..eti muhusika jina linahifadhiwa..najua ni habari ya uongo na majungu tu
 
Back
Top Bottom