Mapya DAWASCO: Mzalendo aliyeibua wizi wa maji wa bil.2 atimuliwa kazi

Status
Not open for further replies.

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009
MAPYA DAWASCO: ALIYEIBUA UFISADI WA BIL.2 ULIOFANYWA NA STRBAG AFUKUZWA KAZI.

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Cyprian Luhemeja limemfukuza kazi mzalendo aliyeibua wizi wa maji ya DAWASCO uliofanywa na kampuni ya STRABAG iliyojenga barabara ya mabasi yaendayo kasi kutoka kimara hadi Moroko jijini DSM.

Kumbe wizi huo ilikuwa ni dili la Akina Luhemeja na aliyekuwa Mtendaji mkuu kabla yake, mzalendo huyo aitwaye Teresia akiwa meneja wa Dawasco Magomeni kwa kushirikiana na wasamaria wema alibaini kuwa STRABAG imejiunganishia maji kinyume na sheria ambapo mteja yeyote wa maji ya DAWASCO lazima aunganishiwe maji hayo na DAWASCO wenyewe lakini STRABAG iliwahonga maafisa wa Dawasco akiwemo Luhemeja ambaye ni mtendaji mkuu kwa sasa, Jackson Midala, mtendaji mkuu kabla ya Luhemeja na aliyekuwa meneja wa dawasco magomeni kabla ya Teresia.

Teresia alipohamishiwa Magomeni akiwa meneja ndio akaliibua hilo..wakamhonga ili asiseme wakashindwa, wakamtishia kumuua wakashindwa, Luhemeja akaamua kumfukuza kazi.

Je, kwa style hii tutafika? Kama wazalendo ndio wanaoshughulikiwa wanabinywa na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa?

Magufuli tuokoe nchi inatafunwa mno. Kama haitoshi luhemeja anajigamba kwamba yeye ni kijana wa mjini ana mtandao hadi ikulu...

===========
UPDATE:

Maoni ya Mdau huyu yamepelekea mjadala kufungwa:

Kwanza nitoe ufafanuzi mchache kwa wale wanaodhani huyo binti anayeitwa Theresia alifukuzwa kazi.

Ukweli wa mambo ni kuwa alikimbia kazini mwenyewe!

Tukianza kurudi nyuma mara baada ya Waziri kuja na tuhuma za wizi wa Maji Strabag wafanyakazi 11 walituhumiwa kuhusika na kashfa hiyo ambapo wapo Mameneja wa kipindi cha nyuma nao walitajwa kama vile Bwana Mvano... Bwana Cha cha pamoja na ndugu Kapera.

Maagizo ya Waziri ilikuwa hawa watu wasimamishwe kazi mpaka tume itakapochunguza na kuleta taarifa kamili kwake. Hivyo wafanyakazi 11 walisimamishwa kwa muda wa miezi kadhaa kupisha uchunguzi.

Kipindi chote hicho walikuja kuchukua barua zao za kusimamishwa na barua za kuwataka kuja kutoa maelezo yao kwenye tume iliyoundwa na mh waziri.

Hapo sasa bi teresia hakitokea kuchukua barua wala kuja kutoa utetezi wake na hata alipokuwa akitafutwa kwa simu ilikuwa haipokelewi. Sasa mtu anatokea na kusema kasimamishwa kazi. Je, tujiulize kwa kosa gani kama tu hajatoa ushirikiano kwa mwajiri wake au hiyo tume.

Pili baada ya kuondoka kazini bi teresia ilikuja kubainika alikuwa anafanya mchezo mchafu na aliyekuwa afisa fedha wake ndugu Fredrick Mapunda. Mchezo huo ulikuwa wa kula pesa kiasi cha Sh. Milion 25 kutoka jengo la Ubungo Plaza. Mpaka sasa hao watu wanatafutwa na Polisi kwa mahojiano zaidi.

Aidha, tujiulize kama huyo mtu hakuwa na hatia, kwanini aliondoka bila kumuaga muajiri wake? Kwanini hakutoa ushirikiano kwa tume iliyoundwa na waziri?

Wadau, tuwe makini na watu wanaofanya makosa na kutaka kutafuta huruma za wananchi kumbe walikuwa wakiwaibia wananchi haohao.
 
Niliwah kuwajulisha Dawasco kuwa Kuna mteja anawaibia MAJI kwa miezi sita , huku akiwa na miradi mikubwa ya kutumia MAJI mengi, kilichotokea Dawasco wakaenda wakapiga pesa ndani ya Sikh mbili wakamfungia Mita akawa mteja halali. Wakati mwingine hakuna haja ya kufuatilia sana mambo ya watu , ni vyema kuangalia ugali wa watoto wetu.
 
Niliwah kuwajulisha Dawasco kuwa Kuna mteja anawaibia MAJI kwa miezi sita , huku akiwa na miradi mikubwa ya kutumia MAJI mengi, kilichotokea Dawasco wakaenda wakapiga pesa ndani ya Sikh mbili wakamfungia Mita akawa mteja halali. Wakati mwingine hakuna haja ya kufuatilia sana mambo ya watu , ni vyema kuangalia ugali wa watoto wetu.
Hiyo ulikuwa umewapa deal. Nchi hii rushwa haitopungua
 
Niliwah kuwajulisha Dawasco kuwa Kuna mteja anawaibia MAJI kwa miezi sita , huku akiwa na miradi mikubwa ya kutumia MAJI mengi, kilichotokea Dawasco wakaenda wakapiga pesa ndani ya Sikh mbili wakamfungia Mita akawa mteja halali. Wakati mwingine hakuna haja ya kufuatilia sana mambo ya watu , ni vyema kuangalia ugali wa watoto wetu.

Duu umeeleweka ndugu, Hata Rais anapoamua kuwashughulikia watu wa aina hii bila huruma tusipige kelele maana tumekua mstari wa mbele kuanza kuwaonea tena huruma.
 
Kama ni kweli basi hata huyo Luhemeja hayuko Salama ataondoka, tuwe watazamaji ni suala la muda tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom