mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Mods naomba msiunganishe huu uzi
Hongera kwa Kuandika vitu vyenye nia chanya juu ya changamoto ya nchi yetu.
ZIFUATAZO NI CHANGAMOTO/MAPUNGUFU NILIZOZIN G'AMUA KWENYE BANDIKO LAKO ZURI.
ZAWADI YA JUMAPILI KWA MH. RAIS JOHN POMBE MAGUFULI
Mambo mengi unayosema yako kihisia..
1:Una chuki na CCM, Sijui kama unachuki na CCM au wanaCCM baadhi, Maana CCM kama taasisi na Misingi yake Ikisimamiwa katika Default zake haina tatizo kabisa. Ni sawa Useme Unachuki na BIBILIA kwa Sababu wakristo ni waovu au ndio wamesababisha Matatizo. Kumbe inaweza kuwa ni Ukengeufu wa wakristo sio bibilia. Huo ndio uelewa wangu kuhusu CCM. Kipaumbele cha Rais ni VIWANDA na hajawahi kuhama naona Utekelezaji wa Majukumu yake unaita Vipaumbele.
2:Mikataba Mibovu, Tunalia watanzania kuwa Mikataba mibovu, Inatunyonya. Zote hizi ni hisia maana mikataba yenyewe Hatujaiona, Na ubovu wake au Uimara wake hatuujui pia Isipokuwa waliosign na wenye access nayo. Badala ya kulia Mikataba Mibovu kwa hisia, Moja Tumuache Rais ambae nadhani anaaccess nazo na anania chanya na taifa apitie ajue nini cha kufanya na kama ni mibovu au sio mibovu. Pili ili kuepuka kuhisi, Tumuombe Rais na Bunge letu Lipitishe Sheria ya Trasnparency au Partial Transparency ya Mikataba ya Rasilimali pendwa kama madini na Gesi. Hapo Tutakuwa tunalaumu based on facts. Sisi sio wa kwanza kwa mikataba ya aina hiyohttps://www.jamiiforums.com/threads/rais-magufuli-mikataba-yote-iwe-wazi-au-nusu-wazi-itapunguza-surprise-nyingi-kama-hiyo-ya-makontena.1224026/
3:Sina Uhakika wa Hizo asilimia za Madini/Ore grade kwa hiyo migodi unazitoa wapi maana geita, wana grade tofauti na ore yao ni tofauti(Oxide Ore), Buzwagi na Buly (Sulphide Ore) na grade zao zote zinatofautiana huku grade ya Buzwagi ikiwa ndio ya mwisho na ndogo. Hii ni kwa Mujibu wa geologists.
4:Basis ya Makadilio yako hadi ukafikia hizo tani za dhahabu(1/4 ya 50,000 tons) umeitolea wapi. Hapo napo panasindikizwa na hisia ya kwamba tunaibiwa. Hadi sasa Ukweli uliopo kabla hatujapata ukweli mpya au Taarifa ya wataalamu Maprof wa Rais ni kwamba. Kila kontena lina wastani wa mchanga tani 20-25, asilimia ya concentration ya dhahabu ni 0.02 -0.05 ambayo inasemekana kuwa ni kubwa kulinganisha na concentrate nyingi duniani na ndio maana wawekezaji wanasema hiyo inachangia karibu 90% ya mapato kutoka kwenye mauzo ya huo mchanga wote na sio Copper kama migodi mingine ya cupper. Hivyo basi utapata kila kontena lina wastani wa kilo 4 hadi 5, na ambayo kwa tan 50,0000 wenda ikawa 2Tons ambazo hupimwa kwa OUNCES. Sio kidogo ni mabillion ya pesa. Hizi ni kwa mujibu wa wawekezaji,Tume iliyowahi kuchunguza kuleta smelter hapa nchini, na watu wanaofanya hiyo kazi huko. Hadit tutakapopata taarifa mpya za Kiuchunchunguzi ndio tutafuta haya na kuweka elimu mpya based on facts and testings.
5: WAJENGE SMELTER WATATUKATA KWENYE Mrahaba? Mrahaba ulikuwa 3% na baadae tukauongeza 4% na mtambo ni wa mabilioni. Ni pesa kidogo mno ukisema watukate maana yake sisi ndio hata madini yatakuwa hayana faida kabisa. Inawezekana Kujenga Smelter yenye hiyo capacity watu wetu wakitafiti na kuja na majawabu kutoka huko dunia ya madini. Mimi pia Nampongeza RAIS kwa KUMTUMA CAG, Wwao wanasema Wataanza Kulipa Cooperate Income Tax baada ya Kutimiza pesa yao waliowekeza ambayo kwa mahesabu yao WATATIMIZA 2019, na ndio maana Juzijuzi walitoa Inadvance Cooperate Tax ambayo wanapaswa kulipa kuanzaia 2019. Wenda CGA akagundua wanatudanganya Wamesharudisha Pesa yao na Badala ya Kulipa Mrahaba 4% waanze Kulipa Cooperate Tax ambayo ni kama 30%. Hapo Tutaandamana Kumpongeza Rais maana hadi sasa anastahili pongezi.
6:Baada ya Katazo la Rais (ANASTAHILI PONGEZI NYINGI), Mambo mengi yamegundulika ambayo bila katazo tungeendelea kuwa Gizani. Kwanza Tutapata Ukweli pili Wawekezaji watajua Nchi hii sio ile walioingia wakiona kila kitu hata kama sio chema kinawezekana. Mfano Mule kuna Madini mengi zaidi ya Copper/Gold/Silver kitu ambacho kilikuwa hakieleweki sana. Tatizo linakuja wawekejazi wanasema ni kidogo sana, Tena hata wao sio mali yao. All byproducts inabaki kama mali ya Smelter. Kumbe wakijenga hapa badala ile kubaki mali ya mchina/Mjapani au Mjerumani inabaki hapa inakuwa processed hapa na tunapata faida. Hiyo kidogo hatupaswi kuambiwa ni kidogo tu bali Tukathibitishe hukohuko hata kama vipimo huku ni vinaonyesha ni kidogo, Na tudukue huyo smelter anafaidika vipi. Tukigundua anafaidi na Hatuna Uwezo wa kuijenga hapa. Tunayafufua nayo yote hata kama ni kumi yaingizwe kwenye mkokotoo wa kodi.
Changamoto hatujui Wawekezaji na huyo Mchenjuaji huko nje wanamkataba gani? Tuko gizani.
Mapendekezo.
1: Tulilie Transparency ya mikataba au angalau iende kwa wakilishi wetu, Hii itaondoa hisia nyingi ambazo wenda hazikuwa na sababu. Amani Itamuongezea Trust muwekezaji kwa jamii ya kimataifa na watu wanaomzunguka/Wananchi
2:Tutrain watu Competent kwenye mambo ya mikataba na Negotiation za kimataifa kama ulivyopendekeza.
3:Wawakilishi wetu wajitahidi kuwa na Taarifa sahihi juu ya mambo yanayoendelea katika maeneo yao, Kiongozi wa eneo husika hajui hata kama huwa kuna copper au kwa nini kuna mchanga buzwg/Buly na sio Geita. Unakuta mbunge jimbo linamgodi lakni anaongea vitu ambavyo inaonyesha Hajui chochote kinachoendelea kuhusu wawekezaji eneo lake. Sasa unategemea huyu atawalisha nini wananchi wake kama sio vitu vya kuhisi. Tujue normal operations ili tuwe na uwezo wa kuidentify abdnormal operations.
Mwisho naungana na Wewe Kumpongeza Rais kwa kuvalia njuga mambo makubwa yenye utata lakini yanafaida kwa masikini,wasio na ajira, walemavu,wajawazito wasio na zahanati. Hili hata kwenye record mbinguni litaingia na tutalielewa zaidi siku akiondoka.
mkulima mwenzako katika tafakuri shambani...,
Ninakubali kukosolewa,kupingwa,kusahihishwa,kukemewa,kupongeza au kurekebishwa katika maoni yangu juu ya bandiko lako...
CCYeriko Nyerere