Maprofesa wa aina hii wanairudisha nyuma Tanzania

Maprofesa wa aina hii wanairudisha nyuma Tanzania

Joined
Jan 16, 2012
Posts
25
Reaction score
15
Ili nchi iweze kuonekana kuwa imeendelea, ni lazima kuwe na viashria vya maendeleo hayo. Viiashria hivyo vyaweza kuwa vingi lakini vipo vya msingi kama vile uwezo wa nchi yenyewe kuweza kufadhiri bajeti yake yenyewe bila kutegemea wahisani ama misaada toka mataifa mengine, uwezo wa kumudu huduma za jamii kwa wananchi wake kama vile afya, elimu, maji, umeme, barabara n.k, uwepo wa haki za binadamu na uhuru wa watu n.k.

Nchi zote zilizofikia ustrawi katika mambo tajwa hapo juu(kama vile nchi za Scandinavia, Ujerumani, USA, UK, Netherlands n.k) zimeweza kwa sababu ya kuwa na wataalamu wanaofikiri vizuri katika kufanya tafiti na kuishauri serikali (wanasiasa) na kuwa na sera nzuri za kutumia rasilimali zinazopatikana nchini ili kujiletea maendeleo.

Lakini pia na wanasiasa wanaowajivika kuwatumikia wananchi waliowachagua iliwasaidia. Haya yote katika Tanzania yetu yamekuwepo kwa kiasi kidogo ama hakuna kabisa. Hivyo nashawishika kusema kuwa kwetu sisi kupata maendeleo itatuchukua muda mrefu ikibidi hata vizazi na vizazi.

Najua utajiuliza, ni kwa nini nasema yote hayo?. Juzi (22 March, 2013) nilihudhuria mhadhara (Public Lecture) ilioandaliwa na Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwashirikisha wanazuoni na wanafunzi katika taaluma za Uchumi, Maendeleo na Siasa chuoni hapo.

Muwasilishaji wa mada alikuwa ni Profesa Johaness Urpelainen kutoka chuo kikuu cha Columbia, USA. Mada iliitwa "The governance of club goods: Improving off-grid electrification in rural India, with lessons from Tanzania". Kimsingi, mada hii ilikuwa ni utafiti wake alioufanya huko India kubaini ni kiasi cha wahindi wangapi hususani wa vijijini hawapati umeme kutoka gridi ya taifa na namna gani ya kuwasaidia waondokane na janga hilo ili waweze kukuza uchumi wao.

Alibainisha kuwa ni zaidi ya 60% ya wananchi hawapati umeme, hivyo akapendekeza kitu kinaitwa "Microgrid electrification"(yaani umeme mdogomdogo) kwa kutegemea jua, upepo, maji n.k. na kuwa tayari mradi huo ushaanza huko India na umefanikiwa.

Baada ya presentation yake, Johaness aliwashauri wasomi wa Tazania kuiga mfano huo kwa kuufanyia utafiti na kuishauri serikali ili iwasaidie wananchi vijijini​ wajikwamue na umaskini.

Profesa mmoja wa Uchumi anayeheshimika chuoni hapo alionesha nia ya kutekeleza ushauri huo na ninamsifu kwa ahadi hiyo (ikiwa ataitekeleza lakini).

Kitu kilichonisikitisha sana ni pale mtaalamu huyo alipouliza kama kunawezapatikana wafadhiri kusaidia kifedha.....Johaness kwa kejeri akamjibu kuwa kuna makampuni ya kijerumani yanajishughulisha na miradi hiyo.

Kimsingi nilikata tamaa ya maendeleo katiaka taifa hili ambalo 10% tu vijijini ndio wanapata umeme ila tuna rasilimali kibao kuliko viinchi vidogovidogo tajiri kama Norway, Denmark, Switzerland etc.

Rai yangu ni kuwa ikiwa hawa wataalamu(maprofesa) wetu tunaowategemea kufikiri ni namna gani ya kutumia resources tulizojaliwa kama gas, madini, ardhi etc wanaumwa kasumba (kama sio kansa) ya kutegemeaa wafadhiri, je tutafika??
 
Kazi ipo,vipi muda wote alikuwa makini au kakurupuka kutoka usingizini,uchovu wa kazi kwa hiyo hana muda wa kupumzika,sasa ili aonekane yupo ndo akauliza hicho alicho kiuliza?????
 
kazi ipo,vipi muda wote alikuwa makini au kakurupuka kutoka usingizini,uchovu wa kazi kwa hiyo hana muda wa kupumzika,sasa ili aonekane yupo ndo akauliza hicho alicho kiuliza?????
tuna kazi kubwa kutatua matatizo hapa tz ukiwemo umeme vijiji. Tanzania is endowed with a milliard of natural resources which can effectively be used to generate power be it hydro power, solar or recycled waste materials. The problem is we tanzanians are lazzy and too individualistic in life style
 
Nafikiri ni aibu kubwa sana Professor kuhusishwa na ufisadi. Nategemea ukishakuwa Professor unakuwa na uwezo mkubwa wa kuchambua mambo na heshima mbele ya jamii. Imekuwa ni kitu cha kawaida miaka ya hivi karibuni maprofessor kuingia kwenye siasa na kuacha kufundisha vyuoni na kufanya tafiti. Kutokana labda na uprofessor wao huko serikalini watapewa nafasi nyeti za uongozi. Sasa kinachotokea ni nini!!, Kwanza huyu professor alisota sana mpaka akawa professor huku akipewa mshahara mdogo sana ambao haukumfikisha popote kimaisha (mshahara wa Professor kwenye vyuo vyetu hapa nchini ni sawasawa na michahara ya vijana wadogo wenye degree moja tu kwenye taasisi mbambali hapa nchini kwenye professional hiyo hiyo). Sasa mpaka uwe professor hapa TZ lazima umri umekuwa umekwenda kwelikweli, miaka 50 na kuendelea. Ukiangalia mpaka umefikisha 50 na uProfessor wako hujafanya kitu chochote kimaisha ukilinganisha na watu wengine ambao waliishia kufanya kazi kwenye taasisi zingine bila kusoma sana. Sasa huyu Professor akibahatika kupata nafasi kubwa mfano kama uwaziri akiwa na miaka 50 unategemea nini, lazima atumie usomi wake vizuri kupiga pesa za kutosha kwa muda mfupi. Habari ndio hiyo!!.
 
Back
Top Bottom