Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,814
- 34,195
Leo tunapika wali wa nazi, viazi vya kukaanga, mchemsho wa mboga za majani na samaki za kukaanga.
Mahitaji:
Tuanze na wali wa nazi
Mahitaji:
- Mchele
- Tui la nazi
- Chumvi
- Viazi
- Kitunguu maji
- Zucchin
- karoti
- French beans
- Samaki
- Tangawizi
- Vinegar
- Ndimu
- Pilipili manga
- Mafuta ya kupikia.
Tuanze na wali wa nazi
- Tayarisha maji yenye tui la nazi na chumvi kidogo na uweke kwenye moto
- Osha mchele tayari kwa kupikwa
- Kabla maji hayajachemka, na yakiwa yamepata moto sana, ingiza mchele uliyo oshwa ndani ya sufuria
- Pika wali katika moto mdogo hadi uive
- Epua wali wako tayari kwa kuliwa.
- Menya maganda ya viazi
- Osha viazi tayari kwa kupikwa
- Weka viazi ndani ya sufuria yenye maji, chumvi kidogo na vitunguu tayari kwa kuchemshwa
- Chemsha viazi kiasi
- Epua viazi vyako na chuja maji uliyochemshia
- Chukua kikaangio na weka mafuta ya kupikia
- Kaanga viazi vyako mpaka vibadilike rangi ya brown na kuiva vyema
- Epua viazi vvyako tayari kwa kuliwa.
- Chukua zucchini, karoti, french beans na giligilani
- Katakata vipande vilivyo sawa
- Viweke ndani ya sufuria na maji kiasi na chumvi kiasi
- Chemsha kiasi na hakikisha visiive sana.
- Safisha samaki vyema
- Katakata vitunguu swaumu na tangawizi na kisha viponde
- Katakata samaki kisha vichane kidogo kidogona kisu kuruhusu mchanganyiko uingie ndani ya samaki
- Changanya Vitunguu swaumu na tangawizi vilivyopondwa na ndimu, mafuta ya kupika, vinegar pamoja na vipande vya samaki
- Acha mchanganyiko huo uingie ndani ya vipande vya samaki kwa muda wa dk 30 - 45
- Weka mafuta ya kupikia ndani ya kikaango na yaache yapate moto wa kutosha
- Ingiza vipande vya samaki ndani ya mafuta na kaanga mpaka vipate rangi ya brown na viive kabisa
- Epua samaki wako tayari kwa kuliwa.