VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,870
Yasingekuwa hayo,muda huu tungekuwa tunazungumza vingine. Mkuu kaagiza ifanywe tathmini juu ya kuporomoka na kupokwa kwa viti vingi kwa CCM katika kila kona ya nchi. Ingawa CCM ina ushindi wa jumla,matokeo haya hayatasahaulika.
CCM imepoteza zaidi ya kupata. Imepunguzwa nguvu hasa strategic areas. Nilipokuwa naripoti toka Mtwara,Lindi,Ruvuma,Iringa,Morogoro na Pwani nilibezwa. Kiko wapi sasa makada wenzangu?
Mapingamizi yametuokoa. Amini nawaambia,katika sehemu zilikopigwa kura,CCM haina wingi wa ushindi. Nyaraka za kiuchaguzi zinazoendelea kumiminika hapa Ofisi Ndogo Lumumba zinathibitisha jambo hilo.
Mkuu kaagiza ifanywe tathmini na kujua tumejikwaa wapi. Kijulikane kilichowachagiza watanzania wafanye walivyofanya. Halafu,hatua zichukuliwe. Na chama kisonge mbele kikisubiri kutetea ubingwa mwakani.
Bila ya mapingamizi,kusingekalika CCM. Asante Mapingamizi kwa kutusitiri!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam