Chama tawala CCM ni chama kinachokufa katika siasa za Tanzainia. Uchaguzi mkuu wa 2010 na uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 umeonesha hivyo. Ni hulka kitu chochote kinachokufa kupigana kuzuia kifo chake. CCM nacho kama chama kitapigana kuzuia kifo chake. That is the law of natural death, hakuna kitu ambacho kinaweza kwenda kinyume na sheria hiyo. Kwa hiyo CCM kitapigana kuzuia kifo chake. Kitatumia mbinu haramu na halali kuzuia kifo chake.
Kwenye mbinu halali inaonekana CCM kwasasa kimezidiwa kete na UKAWA. Hivyo CCM 2015 kitagemea mbinu haramu kushinda uchaguzi. Wote tunajua CCM sasa hivi sio tena chama cha siasa, bali ni chama dola. Ushindi wa CCM unategemewa sana dola. CCM leo ikinyang'anywa dola basi itakufa kifo cha mende.
Mojawapo mbinu haramu ambayo CCM wanaitumia ni kuwawakea mapingamizi wagombea wa UKAWA, ili mwisho kwa kushirikiana na dola, wagombea hao wa UKAWA huenguliwa na wagombea wa CCM kupita bila kupingwa. Mbinu hii haramu imeonekana kuinufaisha sana CCM kwenye uchaguzi wa S/mitaa 2014. Ni mjinga tu ndiye atashindwa kufahamu kuwa mbinu hii CCM wataitumia tena kwenye uchaguzi mkuu 2015. Je, UKAWA wamejifunza nini kutokana na mbinu hii haramu ya CCM?
Je vyama vya UKAWA vimejipanga vipi kukabiliana na mbinu hiyo haramu ya CCM 2015. Dr. Slaa 2015, akitutangazia kwamba amekamata mawasiliano ya Kinana akiwaelekeza wagombea wa CCM nchi nzima kuwawakea mapingamizi wagombea wa UKAWA that will be no brainier! Kwasababu hilo ni jambo ambalo kila mtu makini analitegemea. Wote tunafahamu by then Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Makamba alivyowalekeza wagombea wote wa CCM nchi nzima walioshindwa uchaguzi wa 2010, kufungua kesi za kupinga matokeo mahakamani na kwamba CCM itawapa support.
Wakati Dr. Slaa atakapo tutangazia kushika hayo mawasiliano ya Kinana, kama inavyotegemewa tunataka pia atueleze ni mikakati gani kama UKAWA wamejipanga kupambana na huo uharamia wa CCM. Kama UKAWA wako makini inabidi hiyo mikakati waianze kuipanga leo na sio kesho. Kukiondoa chama tawala madarakani sio lelemama hata kama una supoort ya 99% ya wananchi.
UKAWA inabidi kuanziia leo wakusanye mapingamizi yote waliyowekewa na CCM katika S/mitaa nchi nzima na kuanza kuyachambua case by case. Yapo mapingamizi mengine genuine kabisa waliwokewa na CCM kutoka na udhaifu wa viongozi wa UKAWA. Pia yapo mapingamizi mengine ambayo yalikuwa ni VIOJA tu, lakini wagombea wa UKAWA wakaenguliwa ili kuipa CCM ushindi wa mezani
Chama Makini ni kile kinachokubali mapungufu yake na kuyafanyia kazi. Hivyo kwa yale mapingamiza ambayo yalikuwa genuine kabisa, lazima UKAWA wayafanyie kazi na kuya address ili yasijitokeze tena kwenye uchaguzi mkuu. Nitatolea mfano wa pingamizi genuine ni kama pale wagombea wa CHADEMA walipogongewa mhuri uliondikwa CDM badala ya CHADEMA, hili ni kosa kubwa sana kisheria CDM is not equivalent to CHADEMA before the court of law. Pingamizi ambalo ninaliita ni KIOJA lakini wagombea wa UKAWA wakaenguliwa ni kama lile eti mhuri waliogongewa wagombea wa UKAWA wino wake umefifia. Hili pingamizi lilikuwa ni KIOJA.
Kubadilisha sheria ambazo hazitaruhusu mgombea kupita bila kupingwa, au kupigiwa kura ya NDIYO na HAPANA kama atakosa mpinzani, ni wazo zuri sana. Lakini kulingana na political landscape za nchi hii ambapo CCM kwanza ndio wanaounda serikali na pili CCM ina out right majority kwenye bunge la JMT. Hili wazo UKAWA walifute kabisa vichwani mwao. Ni ndoto za UTOPIA kudhani serikali ya CCM kwanza inaweza kuleta mswaada kama huo bungeni, lakini hata kama ikiuleta wabunge wa CCM wataupitisha, that will be like shooting themselves (CCM) on their feet.
Mojawapo ya mbinu haramu wanazofanya CCM na mtu yeyote makini anafahamu fika kwamba CCM watazirudia tena 2015, ni kuwahonga wagombea wa upinzani last minutes na wagombea kujiondoa. Kuteka wagombea wa upinzani siku ya mwisho ya kurudisha fomu. Wakurugenzi ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi kukimbia ofisi zao siku ya mwisho ya kurudisha fomu ili kukwepa kupokea fomu za wagombea wa upinzani.
Ili kukabiriana na mbinu hizo haramu nilizozitaja hapo juu, UKAWA inabidi watoe time table ya kurudisha fomu kwa wagombea wake wote nchi nzima. Hiyo time table iwe allowance ya wiki moja kabla ya siku ya mwisho ya kurudisha fomu iliyowekwa na NEC. Ili kama itatokea mgombea wa UKAWA aidha amerubuniwa, ametekwa, mkurugenzi amekimbia ofisi kukwepa kupokea fomu ya mgombea wa UKAWA basi uwepo muda wa kutosha (1 week) kurekebisha makosa hayo.
UKAWA wasikubari kabisa wagombea wao 2015, kurudisha fomu siku ya mwisho ya kurudisha fomu. Kukubari huo ujinga itakuwa ni sawa na mtu kuchezea mdomo wa mamba kwa mkono na mtu yeyote makini anafahamu nini mamba ataufanya huu mkono unaochezea kinywa chake.
Merry Christmas
CC. Makene, Ben Saa8, Molemo, Mwita Maranya, Makamanda wote