Mapinduzi katika nchi za Scandinavia na Tanzania yetu

Mapinduzi katika nchi za Scandinavia na Tanzania yetu

Joined
Sep 12, 2012
Posts
18
Reaction score
7
Imekua ni tabia iliyojengeka kwa watanzania na hasa vijana kulilia mabadiliko nchini.. kisiasa, kiuchumi na kijamii., hii imedhihirika mtaani tunakoishi na hapa jamvini (JF). Lakini, je sisi tumebadilika? Nini ungekifanya kama leo ungepewa uongozi?

Kumbuka yale tunayofanya kila siku at an individual level ndio yanayoifanya/yatakayoifanya Tanzania ya kesho. Kesho wewe ndio kiongozi serikalini, kwenye NGO, katibu mkuu/bosi wizarani, kwenye kampuni au bosi katika kitengo nyeti nchini..

swali; Je? Wewe umebadilika?? nini umekifanya/unakifanya kuleta mabadiliko katika jamii inayokuzunguka? (just pale mtaani unapoishi au kazini) What are you doing to help/make a change and positively influence others?

Vijana wengi leo wanafikiria/wanaomba wapate cheo/nafasi nyeti serikalini/wizarani/kwenye kampuni ili na wao wapige (waibe).. wanaita kula kwa zamu.. Haitakiwi kuwa hivyo!!

With this mentality tutafika kweli?? What if everything was fair?? Tanzania bila rushwa, Tanzania yenye upendo na kujaliana.. Kila mtu katika nafasi yake anafanya kazi yake, anatimiza wajibu wake ipasavyo kwa haki, usawa na kujali wengine.. Kwa nini kuuendekeza ubinafsi?? Itakufaidia nini kupata mafanikio ya muda mfupi at the expense of our fellow poor citizens., kwa sababu kila shilingi unayoiba, rushwa unayotoa na kupokea., wajibu unaoshindwa kuutimiza unasababisha kifo, uadui, kupotea kwa upendo kati yetu na hali ngumu ya maisha kwa watanzania wengi..

-->TUBADILIKE NDUGU ZANGU, SOTE NI NDUGU.. Tafuta uongozi kwa lengo la kuleta mabadiliko na kuwasaidia wengine and in return utapata maisha mazuri na ya kuridhika kimwili na kiroho (complete satisfaction take an example of mwl. Nyerere)..

**INAANZA NA SISI VIJANA, Let us all dream for change and make a vow in our hearts!Tunaweza kuwa more than Scandnavia countries taking into account historia yetu ya undugu..
TUBADILIKE KIFIKRA NDUGU ZANGU, LET US BUILD A NEW TANZANIA WITH HOPE AND FUTURE..
It starts with you., with me.. Think positive, find pride in doing good things
 
Vijana wengi wa leo kwa kukosa elimu bora, hawawezi kupambanua na kuchambua mambo yanayotokea katika jamii zao, wanategemea aje mwanasiasa awatatulie matatizo yao!

Ndo maana wanafaninisha vyama vya siasa na timu za mipira za ulaya! Wanaona bora washabikie chama kinachowahonga kofia, T-shirt, vijipesa, khanga nk. wakisaidie kushinda katika chaguzi mbalimbali ili wawacheke wenzao wa upinzani. Hawajui mbinu hizo ndizo zinazo wafanya waendelee kunyonywa na mafisadi bila kujua. Vijana hawa wavivu hawapendi mapambano ya kijinasua kwenye tope la ujinga.

Vijana wa sasa hawajui wajibu wa serikali kwao wala hawajui serikali za mataifa mengine zinawajibikaje kwa wananchi ili kuwaletea maendeleo. Sana sana wanatumika kama punda kubeba unga ili watoke haraka kibinafsi. Nchi imepotea hii!
 
Nakubaliana na wewe Anko sam.,
As a result wengi wanaoingia kwenye siasa ni wachumia tumboni
 
Back
Top Bottom