Mapinduzi Cup: Leo ni Simba na Mtibwa

Mapinduzi Cup: Leo ni Simba na Mtibwa

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,356
Simba na Mtibwa Sugar Leo zitacheza Fainali ya Mapinduzi Cup 2015 kwenye Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.

Hii itakuwa mara ya pili kwa Timu hizi kukutana kwenye Mashindano haya kwani walikuwa Kundi moja na hapo Januari Mosi Mtibwa Sugar iliifunga Simba 1-0 ikiwa ni mwendelezo wa uteja wa Vigogo hao wa Tanzania toka kwa Timu hiyo ya Manungu, Morogoro.

Hata hivyo, Simba baada ya kupokea kichapo hicho ilijikongoja na kutinga Fainali kwa kushinda Mechi zao za Kundi lao zilizobaki kwa kuzifunga 1-0 Mafunzo na JKU na Robo Fainali kuinyuka Taifa ya Jang'ombe 4-0 kisha Nusu Fainali kurudia ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi ya Zanzibar.

Mtibwa Sugar wao, baada ya kuifunga Simba, walitoka 1-1 na JKU na 0-0 na Mafunzo na kwenye Robo Fainali kutoka 1-1 na Azam FC na kuibwaga kwa Penati 7-6 kisha Nusu Fainali walitoka 0-0 na JKU na Mtibwa kusonga kwa Mikwaju ya Penati 4-3.

SokaInBongo
 
Back
Top Bottom