Mapigano kati ya India na Pakistan yauwa raia saba

Bikis

Member
Feb 23, 2019
52
74
MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA YA TV
burger.svg

  1. IDHAA YA KISWAHILI
  2. HABARI ZA ULIMWENGU


Taarifa ya Habari za Ulimwengu kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW


Matangazo
HABARI
02.03.2019 | 15:00
  • Mapigano kati ya India na Pakistan yauwa raia saba
    Wanajeshi wa pakistan na India kwa mara nyingine tena wameshambuliana katika vijiji vya eneo linalozozaniwa la Kashmir na kusababisha vifo vya zaidi ya raia saba na wanajeshi wawili wa Pakistan, kwa mujibu wa taarifa za Jumamosi za maafisa husika. Wakati mvutano huo ukiwa umepamba moto kati ya mahasimu hao wawili wamiliki wa silaha za nyuklia, kauli ya waziri mmoja wa Pakistan ya kwamba huduma ya pamoja ya treni kati ya nchi hizo mbili itaanza tena kufanya kazi Jumatatu, imeashiria huenda hali hiyo ya mapigano ikatulia kidogo. Mvutano umezidi kushika kasi tangu ndege ya India kuingia katika anga la Pakistan Jumanne iliyopita, iliyofanya kile kilichoelezwa na India kuwa ni shambulio la kustukizia dhidi ya wanamgambo wanaohusishwa na ulipuaji wa mabomu wa kujitoa muhanga wa Febuari 14 katika eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India. Shambulio hilo limesababisha vifo vya wanajeshi 40 wa India. Pakistan ililipiza kisasi, kwa kuidungua ndege ya kijeshi Jumatano na kumshikilia rubani wake, ambae baadae alikabidhiwa kwa serikali ya India Ijumaa kama ishara ya kutaka kurejesha amani...source bbc
 
Back
Top Bottom