Mapharao waitibulia Tanzania FIFA

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KIPIGO cha mabao 5-1 ilichokipata Taifa Stars kutoka kwa timu ya taifa ya Misri, Pharaos, kimesababisha madhara makubwa katika ngazi za ubora wa viwango vinavyotolewa na shirikisho la soka la Kimataifa, FIFA.

Baada ya kufanya vizuri katika michuano ya Chalenji, Tanzania ilipanda kwa nafasi nane, kutoka 124 hadi 116 lakini kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa jana na FIFA, Tanzania imeshuka kwa nafasi nne.

Kuporomoka huko ni matokeo mabaya ya kufungwa mabao 5-1 na Misri, sare ya 1-1 na Burundi na ile ya Uganda katika mashindano ya Bonde la Mto Nile yanayoendelea nchini Misri.

Mbali na kushuka nafasi hizo nne, Tanzania bado inashika nafasi ya pili katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati unaosimamiwa na Baraza la Vyama vya Soka ukanda huo, CECAFA chini ya Rais wake, Leodegar Tenga wa Tanzania.

Mbali na Tanzania ambao ndiyo mabingwa wa CECAFA, Uganda inaongoza kwa kushika nafasi ya 83 ikiwa imeporomoka kwa nafasi tatu.

Kenya inashika nafasi ya 125 ikiwa imeshuka kwa nafasi tano, na kuendelea kuwa ya tatu katika ukanda wa CECAFA ikifuatiwa na Rwanda katika nafasi ya 134 ambayo imeshuka kwa nafasi mbili na Burundi katika nafasi ya 140 ikiwa imeshuka kwa nafasi 12.

Nchi nyingine za CECAFA ni Ethiopia ambayo imeng'ang'ania nafasi yake ya 124 wakati Sudan iliyokuwa nafasi ya 92, imeporomoka kwa nafasi nane na sasa inashika nafasi ya 100 huku Eritrea ikiporomoka kwa nafasi moja, kutoka 177 hadi 178.

Somalia imeshuka kwa nafasi tatu kutoka 182 hadi 185 wakati Djibouti imeporomoka nafasi moja kutoka 191 hadi 192.

Orodha hiyo inaonyesha nchi za Afrika ya Magharibi na Kaskazini zimeendelea kufanya vizuri zaidi ya Afrika ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Misri iliyo kaskazini, imeendelea kuongoza Afrika kwa kushika nafasi ya 10 katika viwango vya FIFA , ikifuatiwa na Ghana katika nafasi ya 16, Ivory Coast (21), Nigeria (32), Algeria (36) na Cameroon iliyo nafasi ya 38.

Mabingwa wa Dunia, Hispania wameendelea kushika namba moja katika orodha hiyo wakifuatiwa na Uholanzi na nafasi ya tatu inashikiliwa na Ujerumani wakati Brazil ipo katika nafasi ya nne.

Argentina inashika nafasi ya tano huku Papua New Guinea ikishika mkia katika nafasi ya 203.

Katika viwango vya Fifa mwaka huu, Tanzania imekuwa ikipanda na kushuka kwani mwezi Januari mwaka jana ilikuwa nafasi ya 108, Februari nafasi ya 108, Machi (109), Aprili na Mei (108), Juni (112), Julai na Agosti (111), Septemba 120, Oktoba 124, Novemba na Desemba ilimaliza nafasi ya 116. Januari 2011 imeanza na nafasi ya 120.

Mwezi Februari mwaka 1995, Tanzania ilishika nafasi ya 65 ambacho ndicho kiwango cha juu kabisa ambacho iliwahi kushika, kiwango cha chini kabisa kwake (Tanzania) kuwahi kushika ni nafasi ya 175 ambapo nafasi hiyo hiyo ilikuwa Oktoba 2005.
 
Hivi yule kocha wa kituruki anaechapa vibao wachezaji kama hawaelewi/kufata masharti ana timu kwa sasa ? mi naona muda umefika wa kupata kocha kama yule,tumejaribu Brazil/Denmark wachezaji wetu hawaelewi bado ni vibao/ngumi tu sasa.
 
hawa vijana wetu tatizo lao wanacheza mpira huku wanajiangalia mara mbilimbili ili mradi tu auze uso wamuone kuwa anajua kucheza, mtu anashindwa hata kutoa pasi sasa utamfundishaje, mtawalaumu makocha bure ila tatizo kubwa lipo kwa hawa vijana hawajitumi na wengi wao wanachukulia mpira ni ustar na sio kazi, kwa hiyo unakuta anawika leo kesho hakuna kitu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom