Maphamasia( pharmacists) pitien uzi huu

odbg

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Posts
318
Reaction score
154
Jamani naomba kujuzwa nini hasa kazi ya maphamasia,fursa sake za ajira na hali halisi ya ufanyaji wa kazi kwa maphamasia Hapa Tanzania
 
Nadhan kaz yao namba moja ni Mahospitalini, mshahara wao inaanzia 980,000. (sina uhakika)

Ajira zao nyingine zipo viwandani, na kwa hii serikali ya viwanda, huenda wakawa na soko sana.

Ngoja waje wenyewe..!!
 
Mfamasia
: Anafanya kazi kwenye drug regulatory authority kama TFDA kwa kuhakikisha dawa zinazotengenezwa na kuingizwa ni salama,zina ubora na zinafanya kazi vizuri

: Anafanya kazi hospitali kwa kutoa taarifa kuhusu dawa kwa health care professionals wengine,kutoa dawa na kuhakikisha dawa zinatumika vizuri na mgonjwa

: Anafanya kazi kwenye community pharmacy kwa kusikikiliza direct complaints na kutoa dawa zisizohitaji prescription kwa wagonjwa na kuwashauri namna nzuri ya kutumia

: Anafanya kazi kwenye academic institutions,mfano walimu pale school of pharmacy MUHAS ni wafamasia

: Anafanya kazi viwandani kutengeneza dawa,mfano pale Zenufa,Shellys,Keko na vingine kuna wafamasia wengi tu wanatengeneza dawa

: Anafanya research and development of drugs,hii ni kazi yake.Anasoma medicinial chemistry na pharmacognosy ili aweze kugundua dawa mpya.Mfano wafamasia waligundua venom ya nyigu ina anti cancer activity

Kama kuna nilizosahau mtaongezea.Mfamasia ni health care professional mwenye taarifa nyingi kuhusu dawa kuliko mwingine yoyote kuanzia nature,mechanism of action,indication,contraindication,adverse effects,drug drug interactions,food drug interactions,etc etc etc

Mfamasia ndio mshauri wa daktari(bongo a pharmacist can not prescribe) kuhusu dawa,hivyo baada ya diagnosis,dokta njoo nikupe best choices ya dawa for that particular disease.

By Ze Heby JF
 
Ana ithibati ya kuuza sumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…