Mapepo hayawezi kuishi nje ya mwili?

Mapepo hayawezi kuishi nje ya mwili?

Ben-adam

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2023
Posts
1,126
Reaction score
2,517
Amani iwe nanyi...

Katika huduma nyingi za kiroho, hasa za maombezi, hushuhudiwa watu wakitetemeka, kupiga kelele, na kutoa sauti zisizo za kawaida ikielezwa kuwa ni "mapepo" yakiongea au kuteseka.

Wakati mwingine pepo husikika "likikiri" limefanya nini ndani ya mtu, huku likidai kuungua au kuteseka kutokana na moto wa kiroho wa maombi. Hili limekuwa jambo la kawaida mno katika huduma za leo na wengi wetu tumeshudia, wala halihitaji nguvu nyingi kuelezea.

Na Katika baadhi ya mafundisho , mapepo huelezwa kuwa yanazurura huku na kule yakitafuta "makazi" ndani ya wanadamu. Hii imejengwa juu ya andiko kama Luka 11:24-26 ambapo Yesu alisema pepo mchafu akifukuzwa, huzunguka katika mahali pasipo maji akitafuta mahali pa kupumzika. Tukizingatia andiko hili:

Ni taabu ya aina gani mapepo hupata wanapokuwa bila makazi? Je, ni njaa, kiu, baridi? Lakini haya ni maumivu ya mwili, si ya roho.

Ina maana mapepo yanahitaji mwili aisha wa binadamu au wanyama) ili yaweze kustarehe? Kama ni hivyo, ni nini cha kipekee katka mwili wa mwanadamu kinachowavutia?

Ni kwa namna gani mapepo yasiyo na miili ya mwili yanaweza “kupumzika” ndani ya mwili wa mtu mwingine? (yanakaa sehemu gani) Je, wanadamu ni "nyumba" za mapepo au kuna usiri wa kina zaidi unaohitaji kufunuliwa?

Wakati wa maombi ya mapepo kufukuzwa, mara nyingi huonekana kama ni pepo ndilo linalozungumza kupitia kwa mtu. Hili linafikirisha.

Je, kiumbe wa kiroho anaweza kutumia mfumo wa sauti wa mwanadamu bila kuwa na mwili?

Kama ni pepo, inakuwaje linaweza kutoa sauti ya kibinadamu, yenye hisia, na mara nyingine hata kutaja majina ya watu au mahali?

Ni nani anayeongea kweli — ni roho ya mtu aliyepandwa au ni sehemu ya fahamu yake ambayo imeathiriwa na mazingira ya kiroho au kiakili?

Tukiwa tumekubaliana kwamba mapepo ni roho, tunabaki na maswali haya:

Roho inaweza kuungua? Ikiwa moto wa kiroho unawachoma mapepo, ni aina gani ya moto huo? Je, ni wa kihisia? Kiakili? Kiimani?

Ni sheria ipi ya ulimwengu wa roho inayosema roho inaweza kuungua? Kama moto ni wa kiroho, basi ni kwa namna gani maumivu hayo yanahisiwa bila mfumo wa neva?

Ni moto huo huo ndio unaotajwa katika jehanamu? Je, ni wa kweli au ni lugha ya picha kuelezea mateso ya kiroho?

KWA NINI MAPEPO HAWATAFUTI ULIMWENGU WAO?
Kama mapepo ni wa rohoni, kwa nini yaishi katika ulimwengu wa kimwili?

Je, kuna “ulimwengu wa mapepo” rasmi ambao unaweza kuwa makazi yao? Kama upo, kwa nini hawaendi huko?

Ni nini kinafanya mapepo yavutike kwa wanadamu kuliko kwa viumbe wengine wa rohoni au mazingira yasiyo ya mwili?

Uzi haulengi kupinga uwepo wa mapepo bali kufungua mjadala juu ya uelewa wetu wa asil yao, jinsi wanavyoishi, wanayoathiri wanadamu, na namna tunavyoelewa maumivu yao, ukiri wao, na mwelekeo wao. Kuna haja ya kuangalia kwa jicho la kiroho na kiakili na tuhoji tusichopenda kuuliza mara nyingi

Karibuni
 
Nimeshaona watu wengi Sana wakiigiza Wana mapepo!
Ngoja wajuzi waje!
 
Duh!
Ni kazi ngumu kukuelekeza, hujui vitu vingi mno hata ambavyo ulitakiwa kujua.
 
Tangu nione clip ya mtu anaamka kwenye jeneza, itoshe kusema watu wengi(sio wote) wanaigiza eti wana mapepo!
 
Kumbuka ule ushuhuda wa Yesu kuwaondoa mapepo mengi kwenye mtu aliuyekuwa akikaa makaburini kwa miaka mingi.

Marko 5 : 1-19

“ 1 Wakafika ng’ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi.

2 Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu;

3 makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo;

4 kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda.

5 Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe.

6 Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia;

7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese.

8 Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu.

9 Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.

10 AKAMSIHI SANA ASIWAPELEKE NJE YA NCHI ILE.

11 Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha.

12 Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao.

13 Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini.

14 Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea.

15 Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa.

16 Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe.
 
Back
Top Bottom