Sisi wana Chadema tuwe kitu kimoja, mawazo yangu nimeyaweka hapa JF kwa vile kwenye vikao vya chama udikteta upo mbele
Waungwana nawasalimia kutoka mashamba ya chai, nipeni nafasi ya kunisikiliza; CHADEMA ni chama kinachonivutia kwa maneno mazuri ya Dr. Slaa na Mheshimiwa Mbowe; kinadharia wana kila sababu ya kupewa nchi.
Hata sisiem wanasema hivi!... Lakini usiku kucha wanapanga mbinu za kuhujumu harakati hizi.
Hatahivyo nimejiunga nacho ndipo nikakuta hali tofauti ndani ya chama wala hakina dhamira ya kuchukua nchi. Matendo ya viongozi waandamizi yanaashiria hawako tayari kuchukua dola 2015, badala yake wametanguliza matumbo yao mbele.
Hela zipi zimeliwa?...
Walipofika Lushoto mwaka 2010 kipindi cha kampeni nilijitolea kwa hali na mali kuwapokea viongozi wetu. Inaniuma sana yale wanayotangaza mikutanoni ni tofauti na uhalisia wa viongozi wetu.
Sijui kama kweli uyasemayo umeyatimiza. Huu ni uzushi. Ni kiongozi gani wa Lushoto umeongea naye. Lete jina tuwasiliane naye.
Hawa hawajashika dola, wanaongoza kwa kutanua kupitia ruzuku ya walipa kodi,wakishika dola itakuwaje???
Ndesamburo, Lema, Mbowe n.k wanatumia kodi uliyotoa wewe?
Uongozi wa juu, hautaki kututhamini tuliyopo mikoani (Nje ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro);
Hizi tuhuma ulizitoa hata kabla hujaenda NCCR... Jiulize kaskazini kuna nini?.. Viongozi wengi wa CCM na mawaziri wakuu wametoka huko - mfano Sokoine, Cleopa Msuya, Sumaye, Lowasa, Mrema (Naibu waziri mkuu)..
Nccr Mageuzi - Mbatia - kaskazini..
Sasa shutuma hizi unatoa wapi? Baki NCCR tuachie CHADEMA.
ruzuku haifiki, ofisi za wilayani zina madeni ya kutisha.
Ofisi ipi iliyo na madeni? Ni kiongozi gani wa wilaya ambaye hajui chadema inafanya nini?.. Mimi ni Mwenyekiti wa wilaya ya Bagamoyo. Tulikaa vikao na kuamua mambo ya kufanyia fedha za chama. Ni mwanachama gani usiyejua ukweli huu?!
Semina elekezi zinapelekwa Arusha, Manyara na Kilimanjaro wanakotoka viongozi wa juu.
Hizi semina elekezi ni wewe unazipeleka ARUSHA? na wewe uko CCM?... Kama ni semina elekezi zilifanyika ngurdoto na Dodoma na kuongozwa na mwenyekiti wa CCM.
Mie nawashangaa elimu ya viongozi wangu jinsi wanavyoitumia; walitakiwa watumie nguvu na raslimali nyingi katika maeneo ambayo chama hakijajikita badala ya kutumia nguvu nyingi kwenye mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
Hivi ungekuwa umefadhili harakati hizi si ungeligawa taifa kwa ukabila wako na ukanda?
NAWAKILISHA KWA DR. SLAA AJITAZAME AKIWA NI MTENDAJI MKUU WA CHAMA CHETU, chama kipunguze kutumia muda na fedha nyingi katika mikoa ya Kaskazini;
Huu uzushi!
tuelekeze nguvu mikoa ya Pwani na Kusini kuna fursa ya kupata wafuasi na wapiga kura CCM huko iko ICU, tusije wapa CUF ujiko.
Hili wazo zuri lisingebebwa na ushabiki wa PM7 aka masalia na pesa za masalia.
Ni ushauri wangu,
Nakutumia namba yangu kwenye private meseji kama una maswali uulize!...
Mkereketwa wa Chadema,
Lushoto
Waungwana nawasalimia kutoka mashamba ya chai, nipeni nafasi ya kunisikiliza; CHADEMA ni chama kinachonivutia kwa maneno mazuri ya Dr. Slaa na Mheshimiwa Mbowe; kinadharia wana kila sababu ya kupewa nchi. Hatahivyo nimejiunga nacho ndipo nikakuta hali tofauti ndani ya chama wala hakina dhamira ya kuchukua nchi. Matendo ya viongozi waandamizi yanaashiria hawako tayari kuchukua dola 2015, badala yake wametanguliza matumbo yao mbele. Walipofika Lushoto mwaka 2010 kipindi cha kampeni nilijitolea kwa hali na mali kuwapokea viongozi wetu. Inaniuma sana yale wanayotangaza mikutanoni ni tofauti na uhalisia wa viongozi wetu. Hawa hawajashika dola, wanaongoza kwa kutanua kupitia ruzuku ya walipa kodi,wakishika dola itakuwaje???
Uongozi wa juu, hautaki kututhamini tuliyopo mikoani (Nje ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro); ruzuku haifiki, ofisi za wilayani zina madeni ya kutisha. Semina elekezi zinapelekwa Arusha, Manyara na Kilimanjaro wanakotoka viongozi wa juu. Mie nawashangaa elimu ya viongozi wangu jinsi wanavyoitumia; walitakiwa watumie nguvu na raslimali nyingi katika maeneo ambayo chama hakijajikita badala ya kutumia nguvu nyingi kwenye mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro. NAWAKILISHA KWA DR. SLAA AJITAZAME AKIWA NI MTENDAJI MKUU WA CHAMA CHETU, chama kipunguze kutumia muda na fedha nyingi katika mikoa ya Kaskazini; tuelekeze nguvu mikoa ya Pwani na Kusini kuna fursa ya kupata wafuasi na wapiga kura CCM huko iko ICU, tusije wapa CUF ujiko.
Ni ushauri wangu,
Mkereketwa wa Chadema,
Lushoto