Mapenzi yanawenyewe

Mapenzi yanawenyewe

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,294
Mapenzi yanawenyewe

Unaweza kuwa mwingi, wa mishanga kuijaza
Ila usifike kingi, mapenzi ukayaweza
Vidogo dogo ni vingi, mwandani kumliwaza
Siwadharau wengine, Mapenzi yanawenyewe

Unaweza kuwa fundi, kiuno kukizungusha
Ila isiwe ni gundi, ya bwana kumgandisha
Au ukampa hundi, na mengi kumuwezesha
Siwadharau wengine, Mapenzi yanawenyewe

Labda umepita veta, upishi ukajifunza
Na viungo ukapata, kipenzi ukamuinza
Bila somo hatadata, ujue na kuikanza
Siwadharau wengine, Mapenzi yanawenyewe

Abuuabdillah ✍️
0744 883 353
 
Back
Top Bottom