Mapenzi yanavyoweza kuchipukia kusikotarajiwa

Jielewe

Member
Jan 10, 2017
38
61
search

Dorcas, msichana wa miaka 30 anayefanya kazi kama Afisa Mikopo kwenye benki moja mjini, hakuwahi kufikiri ingetokea siku moja ‘achepuke’ kimapenzi na Johnson ambaye ni mfanyakazi mwenzake. Miaka mitatu iliyopita wakati anaanza kazi kwenye benki hiyo, Dorcas alikuwa na msimamo thabiti na aliheshimu ndoa yake.

Ingawa alifanya kazi kwa karibu na Johnson, Dorcas hakumchukulia kama mtu mwenye sifa stahiki za kumvutia kimapenzi. Kilichotokea mwaka mmoja baadae, kwa mujibu wa Dorcas, hakieleweki. Dorcas si tu amejikuta kwenye penzi zito na Johnson, lakini amejikuta akichafua sifa yake na kuhatarisha kazi yake.

Maisha ya Dorcas yamevurugwa na kosa moja baya. Kuanzisha mapenzi ofisini. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, mtu mmoja kati ya watatu wanaofanya kazi ofisi mmoja hujikuta akianzisha mapenzi na mfanyakazi mwenzake. Aidha, mtu mmoja kati ya wanane ana uwezekano mkubwa wa kufanya vitendo vyenye vionjo vya ngono katika mazingira ya ofisi.

Ingawa mapenzi ofisini huwaathiri wahusika wote wawili, mara nyingi mwathirika mkubwa huwa ni mwanamke. Kisaikolojia, mwanamke huchukulia mapenzi kwa hisia na uzito zaidi kuliko mwanaume. Pia inapotokea wawili hao wamebainika, jamii yetu humwadhibu mwanamke kwa maneno na hisia kuliko mwanaume.

Sote tunafahamu hatari ya mapenzi kazini. Mbali na kupoteza kazi ukiingia pasipoingilika, unaweza kuharibu sifa yako, ukapoteza furaha ya kazi na hata kuvuruga ndoa/mahusiano uliyonayo. Jambo la kujiuliza, hata hivyo, ni kwa nini watu ambao awali wasingedhani wangejikuta kwenye lindi la mapenzi na wasiyemtarajia, hujikuta katika mazingira ambayo hawawezi tena kujizuia?

Mazoea ya kikazi

Wafanyakazi wengi hujikuta wakijiwa na hisia za kimapenzi na wafanyakazi wenzao kwa sababu ya kutumia muda mwingi pamoja. Dorcas anaeleza jambo hili vizuri. ‘Hata sijui ilikuwaje. Sikujua kinachoendelea hata. Tulikuwa tunafanya kazi pamoja kwa muda mrefu. Nikaanza kupenda kazi yake. Nikaanza kuvutiwa na bidii yake kazini. Basi nikajikuta nampenda.’

Ofisi inaweza kuwa bustani ya mapenzi. Kufanya kazi kwa karibu na kwa muda mrefu pamoja kunaweza kuzalisha hisia zisizotarajiwa kama ilivyotokea kwa Dorcas.

‘Tulifanya kazi kwa karibu sana,’ anasimulia. ‘Unajua kipindi hicho sikuwa nafahamu vizuri kazi. Johnson ndio akawa msaada wangu pale ofisini. Wakati mwingine tulikaa mpaka usiku tukikimbizana na deadline (saa ya kukabidhi kazi)…kidogo kidogo nikaanza kumpenda.’

Pamoja na umuhimu wa kufanya kazi kwa ukaribu na wenzako, ni muhimu kujiwekea misimamo itakayokulinda. Epuka kuweka mazingira ya urafiki wa karibu na wafanyakazi wa jinsia nyingine kama huna ujasiri wa kuutambulisha kwa mwenzi wako au wafanyakazi wengine.

Endelea hapa kwa makala kamili
 
Inategemea mtu na mtu,wengine ndio hivyo makauzu ila kitu kinachoitwa HISIA ni kibaya sana...muda mwingine unajikuta umefall in love bila kujua ilikuaje kuaje
 
Back
Top Bottom