Mapenzi Yanaumiza

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,972
Reaction score
22,922
Kadiri unavyopenda zaidi, ndivyo unavyozidi kuumia. Yule unayempenda zaidi atakuumiza zaidi ikiwa huna uwezo wa kumwacha. Unampenda sana kiasi kwamba unavumilia madhaifu yake yote.

Upendo na maumivu ni mapacha wasioweza kutenganishwa. Jambo lililo chungu zaidi ni pale unapotambua kwamba uliyemchagua awe mpenzi wako na kumweka kama kipaumbele chako kwa muda mrefu, yeye hana mpango wowote nawe.

Kamwe usimpuuze mtu ambaye anakupenda kiukweli. Kamwe usimdhuru mtu kwa makusudi kwa sababu tu amekuumiza kwa bahati mbaya. Jumuumiza mtu, ambaye unajua atakusamehe ni ukatili mkubwa.

Usikimbie uhusiano ili kuepuka kuumia. Wakati upendo una umiza, lakini pia upendo huponya maumivu.

Mabishano, maumivu na migogoro na umpendaye ni jambo lisiloepukika. Ila ikiwa utashikamana, utapata nguvu zaidi.

Hata hivyo, ikiwa unayempenda ataendeleza unyanyasaji, hapo uhusiano utakuwa umevuka mipaka kutoka kwenye upendo hadi kuwa chuki.

Uhusiano ni two ways traffic. IT WON'T WORK IF ONLY ONE PERSON IS PUTTING IN THE EFFORT.

Kusimama peke yako ni bora kuliko kusimama na mtu ambaye anakuumiza kwa makusudi.
IT HURTS TO LET GO, BUT IT HURTS MORE TO HOLD ON TO ABUSE.

Mtu anaweza tu kuendelea kukuumiza ikiwa unamruhusu.

Ubarikiwe.
 
Namaanisha inakulazimu nawe kua na pisi zaidi ya Moja kuhepusha majeraha ya moyo
Nijuavyo mie kumiliki pisi zaidi ya moja ni kujiongezea maumivu tu. Wala hutaponya msjeraha zaidi ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa.
Hivyo kama mmoja amekushinda hao wawili utawaweza vipi?
 
Ukikosea fomula huwa ni kazi ngumu sana kumjua akupendaye
Hakuna formula ya kumjua mtu akupendaye kiukweli kwa sababu kwenye mapenzi kuna watu wanajua kuigiza.
Wakishakujua kwamba akili yako inawaza nini wanapita mlemle unapowaza wewe kwa kuangalia alama za mtu akupendaye.
Utakuja kuujua ukweli baada ya miaka kadhaa kupita huyo muhusika akishatimiza malengo yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…