Pendaneni
Senior Member
- Feb 12, 2014
- 134
- 108
Jamani mapenzi, yananitatiza, Kulala siwezi, kusema siwezi
Chakula sitaki, nakiiona sumu, Mapenzi yamenivaa, nami ugenini
Akili imenipaa, hata njia siioni, Mapenzi yana hadaa, ya kweli nawambieni
Haiba imepotea, uzuri umenitoka, mali imeangamia, maradhi hayakutoka,
Mwenzenu nimepotea, muokozi kanitoka, Enyi wenye ukarimu, siri nawatobolea
Moyo umepata sumu, madawa hayakufaa, Kupenda kitu adimu, nawambia kuna baa
Ya kweli nawambieni, myatie akilini msipende ugenini, mtaingia hatiani
Mtalala majiani , wazimu tele vichwani