Mapenzi yanamtesa sana jirani yangu. Nasikia alinyweshwa maji ya bendera na mke wake

Applicant

JF-Expert Member
Feb 12, 2020
1,962
1,746
Kiukweli kuna jamaa mmoja hapa jirani yangu anateswa sana na mkewake, anapigwa sana kama mtoto lakini hawezi kumuacha huyo mwanamke.

Kuna siku alimuuliza mke wake kua anaenda wapi, halafu ilikua mbele za watu, aisee jamaa alichezea makofi kama mwizi, nguo anafua, vyombo anaosha, jamaa anahitaji msaada.

Kuna story hapa mtaani kua huyo mwanamke alimchanganyia dawa kwenye maji aliofulia chupi, yaani maji yale baada ya kukamua chupi akayamix na dawa za kienyeji ndio maana jamaa hafurukuti.

Kuna wazee hapa mtaani wanasema hakuna limbwata baya kama lakuchanganya na maji yaliofulia nguo ya ndani. Huyo mwanamke kamfanyia jamaa ukatili sana, yani mshkaji kawa mzalendo kwa mkewake kupitiliza, kawa kama zezeta.

Tuwe makini wakuu.
 
Hakuna maji Wala Nini mume kaamua tu yaushe
Siku kaamua kusara heheheh acha tu
 
Kakubaliana na hali.

kama vile maskini anaovyokubaliana na umaskini japo unamtesa.
 
Hakuna maji Wala Nini mume kaamua tu yaushe
Siku kaamua kusara heheheh acha tu
Siku akilisanua ataua hii niliona kwa jamaa flani alikuwa anaishi jirani na nilipokuwa nikiishi naye alikuwa kamahuyo jamaa anayemsema, mbaya zaidi akawa anatembea na jamaa mwingine jirani na hapo ambaye alikuwa kafiwa mke.
Akiamka asubuhi anaenda kwa jamaa anapika anafua anaangalia watoto wake kila mtu anajua kuwa analiwa na mgane huku mmewe anabaki nyumbani anapika anaosha vyombo n.k.
Siku jamaa alipolianzisha hakuna aliyeamini na mkewe akamfukuza kabisa na mgane akamkana basi mpaka leo huyo mama anatangatanga tu .
 
Back
Top Bottom