Mapenzi ya siku hizi
tofauti na zamani Ya sasa yanahirinzi,au kitanzi shingoni Mapenzi ni
kama wizi,ulahai wa moyoni Wapendwao si wajuzi,hawajui kuthamini Wengi
wao ni bazazi,mapenzi ya mdomoni Wamekua km nzi,haweshi vichochoroni
Nami nasema siwezi,hili penzi la kihuni Wanifanyia ushenzi,eti
unanitahini Takuona mpuuzi,kama hujajibaini Kila ninavyokuenzi,hujui
yangu thamani Nenda kwa hao washenzi,wakulao majini