Mi huwa nawaambia wanaume kuwa kamwe usimuonyeshee mpenzi wako wa kike/mke wako kuwa unampenda sana. Mwanamke akishakusoma hivyo atakushika mapembe na wewe kazi yako itakuwa ni kumfuata yeye atakako. Sasa mwenzetu pamoja na vioja anavyofanyiwa anaomba ushauri. Hivi ukifiwa huwa unahitaji kutafuta ushauri kwa watu, kwamba wakushauri labda uzike au upeleke maiti hospitali? Hapo huwa hakuna ushauri, ukifiwa wewe kazi yako ni kuzika tu, sasa huyu kaona mwanamke kabadilika na anaonyesha dalili zote za kupata mwanamme mwingine yeye yuko nyuma ya keyboard kuomba ushauri. Wewe mpige chini na jifanye kama huna time naye tena. Baada ya muda yeye ndio ataanza kukutafuta. Na kama kweli akili zako hazikutoshi utamrudia.(Ni kama nakuona vile). I never commit to women because doing so is harmful to your health!yani wewe na akili zako zote unashindwa kujua..manzi kama hakukubali ukimtell i love u anakwambia ok..ama thanks..jombaa..Jipangeeeeeee warembo wote hawa we unakomaa na long distance? amin kwamba kuna mtu anakula mzigo huo...
Tumekuwa pamoja kwa miaka miwili sasa plus miaka miwili ya kuzungushwa inakuwa minne. Nampenda sana na ndo mtarajiwa wangu Mungu akijalia. Kwa muda wa mwaka mmoja sasa hivi yuko mbali kabisa nami ila navumilia na sijawahi kumcheat. Lakini kuna tabia imejitokeza kama miezi mitatu hivi simuelewi kwa kweli.
Nikipiga simu muda mwingine hapokei wala hata kunitumia msg kwamba yuko busy hakuna, natuma msg hajibu. Kuna wakati akipokea maongezi yake hata nnavyoongea na dada yangu aliyenizidi miaka 25 huwa nafurahia kwani huwa tunataniana. Majibu yake ni mkato na ukimwambia i love you anakujibu, ok! Hii ni tofauti na mwanzo. Nimezoea kila asubuhi na mapema kumsabahi na kumtakia kazi njema lakini siku hizi anapokea cm na kuniambia ana usingizi hata kama ni muda ambao mfanyakazi anatakiwa aamke. Kuna siku ndo kabisa sauti ilikuwa kama kuna breakfast inaendelea, loh!
Nilikata simu na kwenda kufanya mambo yangu. Jana nimempigia simu akawa anaongea kiuoga nikamuuliza, are you at your home? Akakata simu na mpaka leo hapokei. Kuna wakati huwa ananambia simu ni mbovu lakini bado najiuliza mbo wakati mwingine unampigia na kuongea naye? Nifanyeje ndugu zangu? Yaani hata ibada yangu leo imekuwa sio kama kawaida.
Tumekuwa pamoja kwa miaka miwili sasa plus miaka miwili ya kuzungushwa inakuwa minne. Nampenda sana na ndo mtarajiwa wangu Mungu akijalia. Kwa muda wa mwaka mmoja sasa hivi yuko mbali kabisa nami ila navumilia na sijawahi kumcheat. Lakini kuna tabia imejitokeza kama miezi mitatu hivi simuelewi kwa kweli.
Nikipiga simu muda mwingine hapokei wala hata kunitumia msg kwamba yuko busy hakuna, natuma msg hajibu. Kuna wakati akipokea maongezi yake hata nnavyoongea na UNAWEZA SHINDWA ELEWA MAANDISHI,LAKINI HATA PICHA JAMANI?
hapo siyo mapenzi ya mbali ,hapo nimapenzi hakuna mkuu...........kwisha habari yako wewe songa na maisha.
hlf huyo mpenzi wako yupo wapi mpaka unakaa mwaka mzima hamjaonana?
Pole sana,i can imagine maumivu unayoyapata kwa sasa.Hiyo ilinikuta mm j2 iliyopita aisee nashindwa ht kusimulia yaan kanisan hapakukalika ila nashukru angalau sasa nimeanza kuzoea.
Tafuta rafiki aliye karibu naye achunguze.. lkn dalili zote zaonyesha huyo hakupendi.. Jiondoe mapema tafuta atakayekupenda kwa dhati
hizo ni dalili tosha kuwahuyomtu,ame loose interest na wewe.ila uamuziniwako,jaribu na wewe kumpa mapozi vilevile,usijionyeshe kwake kama unaumia.ingawa unaumia,baada ya muda ukiona mambo ndio hayo hayo,songa mbele na maisha yako.mpotezee for good ingawa ni ngumu
Pole maumivu yako ni kutokana na hisia zako. Uwezekano mkubwa ana mtu mwingine tayari.
Kujihakikishia (itasaidia nadhani), nenda kwake utapata ukweli wote na itasaidia kusupport maamuzi yajayo.
Pole sana mpendwa!
asante dada angu. Itabidi nijipange maana yeye kuja ananambia ratiba imemkaba. Lakini unaweza fika kule ukaishia kutambulishwa kwamba huyu ndo mume wangu. Hayo maumivu yake yatakuwa mara nyingi zaidi. Unaweza jikuta unaishia jela kwa kupiga mtu.