Mapenzi ni kama pombe

Mapenzi ni kama pombe

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,042
Reaction score
1,299
MAPENZI NI POMBE

Kwanza yanaingia kwa utulivu kama kinywaji baridi kwenye koo lenye kiu.

Hakikuleweshi mara moja, unajiona uko sawa. Unacheka, unapiga stori, unajibu kwa utulivu.
Lakini polepole… inajikusanya kwenye damu.

Macho yako yanaanza kumtafuta bila kutumwa. Sauti yake inakuwa mziki unaoupenda kusikia kila siku.
Ukimya wake unakuwa kelele kubwa moyoni.

Na kabla hujajua umeshalewa Unashindwa kutulia bila yeye.
Unayumba bila kuguswa, unaanguka bila kusukumwa.

Mapenzi hayakuleweshi mwanzoni… lakini yakikupanda, hakuna anayekuokoa.

Na mtu hakujua kuwa moyo unaweza kulewa kwa kutajwa tu jina la mtu mmoja.

Wengi hawajui kuwa mapenzi unayanywa kama mnazi, ila yakikupanda… unamuita “baby” hata mbele ya watu wazima.

Nguvu ya mapenzi ni kubwa kuliko wimbi la bahari

Hakuna mtu wa kuyakata mapenzi ya mtu kama ambyo huwezi yakata maji

Abuuabdillah ✍️
0744883353
 
Sasa ndugu kitendo cha kutuandikia no yako maana yake tukutafute utupatie hiyo pombe ya mapenzi ama..?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom