Salaam wana jf
Mimi ni miongoni Mwa vijana tunaopambana na hali zetu kwa kujiari kupitia biashara ndogondogo zinazotuwezesha kupata riziki japo kwa nguvu kubwa.
Mwaka 2015 nilihitimu mafunzo ya Ualimu katika chuo kimoja cha serikali, baada ya hapo nilirejea mtaani kwa matarajio tele ya ajira. Nilipo rejea kitaani nilipatwa na unyonge na aibu kubwa baada ya kuona vijana wenzangu waliofeli darasa la wamepiga hatua kubwa kimaisha.
Baada ya wiki mbili nilipata wazo la kwenda mkoani Tabora kusaka fursa, ambako nilianza kufanya vibarua vya kubeba tofali katika kampuni la ujenzi wa ghorofa. Nakumbuka kubeba tofali moja kutoka chini hadi ghorofa ya4 ilikua sh.100, hata hivyo nilidumunayo kwa muda wamiezi 4 tu.
Baada ya hapo nilipata kibarua kingine kama muuzaji wa Duka la vipodozi mjini pale. Kwa kupitia biashara hii nilianza kutengeneza mawazo mbalimbali ya kibiashara kichwani mwangu. Kipato kidogo nilichokua nikilipwa ilikua chachu ya kutamani kujiajiri.
Nilianza kujichanga hatimaye nikaanza mapambano mwenyewe , hali ilikua tete lakini nilishinda hatimaye genge likawa Duka.
Baada ya miezi 7 kama mjasiriamali tena Mwalimu by professional nikapata wazo la kufungua branch ya biashara yangu pembezoni Mwa ya ile ya awali, nilifankisha japo changamoto ilikua kumpata kijana msimamizi mchapakazi na mwaminifu.
Nilifanikiwa kukutana na binti mwenye asili ya kaskazini mashariki mwa Tanzania ambako nami ndiyo home. Binti ilikua mchapakazi kunishinda Mimi, ndani ya muda mfupi aliikuza biashara ile hatimaye akawa mpinzani wangu Mkubwa kibiashara.
MAPENZI:
Binti alianza taratibu tabia ya kunionea huruma kwa kuanza kuniletea chakula hasubui anapokuja kazini, ghafla geto kufua hukubiashara zikishamiri.
Paaaap! [emoji173] [emoji173] [emoji173] mapenzi mubashara.
Baada ya muda mfupi process za ndoa zikakamilika, bonge la sherehe likafanyika.
MAISHA YA NDOA
Maisha yalikua tofauti sana mke hakua mchapakazi tena, alifungua biashara saa5 na kufungua muda apendao.Alianza kua na mashoga kila kona ya mji. Mume sikua na kauli kwa mkewangu, hashikiki hakamatiki. Tulikula tutakacho ila furaha na amani ya kweli vilikosekana.
Alianza kucheza vikoba kila kona hadi nje ya mkoa.
Hatimaye biashara yake ikafifia na kufa[emoji26] [emoji25] [emoji25] [emoji24]
Muda mrefu niliutumia kuwaza kuliko kufanya kazi. Nilianza kuijutia ndoa...
Mashtaka yote niliyo yawasilisha kwao yalichochea matatizo badala ya kutatua.
Nilijuta kila wakati kwakua kulikua na pendekezo la mke wa kumuoa kutoka kwenye familia yangu nikawakatalia.
Sikuweza kuishirikisha familia yangu kwenye mgogoro ule kwa kua niliogopa lawama ya kukurupuka kuoa bila kuchunguza.
Hatimaye niliamua kumpa talaka [emoji174] [emoji181] ,...Nilijiandaa na kusogea hadi Singida, Manyara,Arusha kwa lengo kupoteza mawazo
Ghafla taarifa zimefika home lawama matusi kejeli kunielekea eti nilikua na mtesa mtoto wa watu.
Ilinibidi nifike home kutoa ushaidi wa matatzo ya bint yule.
Wengi walichukia baada ya kuthibitisha ukweli huku wa kidai "hukimrudia hatutakua pamoja nawe".
Nilipoamua kurudi Tabora nilishangaa kuona ,Mtalaka kasafisha kila kitu hata vile visivyo muhusu.
Kushauriana na familia yangu walitaka nisimdai chochote.
Kaniachia maumivu makali sana kwani hats nguo zangu kabeba, tena kwasasa nalala kwenye mkeka.[emoji35] yaani from hero to zero.
Hapanilipo natamani Magufuli atoe ajira nikashike chaki
.Ahsanteni