Mapenzi na Mganga Yasababisha Moto kukolea

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Moto uliolitekeza ghorofa moja nchini Marekani na kupelekea kifo cha mtu mmoja na watu wengine 100 kukosa makazi ulisababishwa na mwanamke aliyekuwa kwenye tamasha la ngono na mganga.
Mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake wa Brooklyn, New York nchini Marekani alimlipa mganga dola 300 ili amuondolee matatizo yanayomkabili.

Mganga huyo naye katika mojawapo ya masharti yake alimtaka mwanamke huyo wafanye mapenzi kwenye kitanda kilichozungukwa na mishumaa, limeripoti gazeti la New York Post.

"Alimwaga pombe iliyotengenezwa kwa miwa kwenye sakafu eneo la mlangoni ili kuzuia mapepo wabaya kuingia ndani, na ili dawa za uganga zifanye kazi, mganga alimtaka mwanamke huyo wafanye mapenzi", liliambiwa gazeti la New York Post.

Huku malavi davi yakiwa yamenoga, kukuru kakara za malavi davi zilipelekea baadhi ya mishumaa kudondoka chini na matokeo yake kuzusha moto mkubwa.

Mganga alijaribu bila mafanikio kuuzima moto huo kwa kutumia maji toka bafuni lakini moto huo ulipozidi kupamba moto mganga na mwanamke huyo walikimbia toka kwenye chumba chao kilichokuwa ghorofa ya nne na kuuacha mlango wazi.

Upepo uliokuwa ukivuma kwa spidi ya kilomita 65 kwa saa uliufanya moto huo uzidi kuwa mkubwa na kuenea kwenye vyumba vingine.

Moto huo uliziteketeza pia vyumba vya ghorofa ya nne na tano na kupelekea paa la jengo hilo kuporomoka.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 62, aliyekuwa akiishi ghorofa ya sita alifariki kutokana na moto huo.

Jumla ya wafanyakazi 200 wa mashirika 44 tofauti ya zimamoto walishiriki kuuzima moto huo na kuuzuia usifike kwenye majengo ya jirani.

Wafanyakazi 25 wa zimamoto walijeruhiwa katika harakati za kuuzima moto huo.

mganga.jpg
 
Utata mtupu huyo mganga kiboko kama pombe ya miwa inazuia mapepo basi tanga wako Salama salimini?@@@@@@!!!
 
Jaman waganga weupe wapo me nilitumika na mmoja alikuwa na mahirizi kabisa na usiku akapata kashfa ya kukaba staff wa kibongo.
 
Moto uliolitekeza ghorofa moja nchini Marekani na kupelekea kifo cha mtu mmoja na watu wengine 100 kukosa makazi ulisababishwa na mwanamke aliyekuwa kwenye tamasha la ngono na mganga.
Mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake wa Brooklyn, New York nchini Marekani alimlipa mganga dola 300 ili amuondolee matatizo yanayomkabili.

Mganga huyo naye katika mojawapo ya masharti yake alimtaka mwanamke huyo wafanye mapenzi kwenye kitanda kilichozungukwa na mishumaa, limeripoti gazeti la New York Post.

"Alimwaga pombe iliyotengenezwa kwa miwa kwenye sakafu eneo la mlangoni ili kuzuia mapepo wabaya kuingia ndani, na ili dawa za uganga zifanye kazi, mganga alimtaka mwanamke huyo wafanye mapenzi", liliambiwa gazeti la New York Post.

Huku malavi davi yakiwa yamenoga, kukuru kakara za malavi davi zilipelekea baadhi ya mishumaa kudondoka chini na matokeo yake kuzusha moto mkubwa.

Mganga alijaribu bila mafanikio kuuzima moto huo kwa kutumia maji toka bafuni lakini moto huo ulipozidi kupamba moto mganga na mwanamke huyo walikimbia toka kwenye chumba chao kilichokuwa ghorofa ya nne na kuuacha mlango wazi.

Upepo uliokuwa ukivuma kwa spidi ya kilomita 65 kwa saa uliufanya moto huo uzidi kuwa mkubwa na kuenea kwenye vyumba vingine.

Moto huo uliziteketeza pia vyumba vya ghorofa ya nne na tano na kupelekea paa la jengo hilo kuporomoka.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 62, aliyekuwa akiishi ghorofa ya sita alifariki kutokana na moto huo.

Jumla ya wafanyakazi 200 wa mashirika 44 tofauti ya zimamoto walishiriki kuuzima moto huo na kuuzuia usifike kwenye majengo ya jirani.

Wafanyakazi 25 wa zimamoto walijeruhiwa katika harakati za kuuzima moto huo.

View attachment 24004

kuna sehemu kwenye hii habari imeelezea kuwa huyo mwanamke au mganga ni ngozi nyeusi?

Hii habari siyo the only source. Sikujibu kwa kutegemea tu hii habari.

Hint: Hizo Brooklyn apartments au project houses mostly ni makazi ya watu weusi.

Pia huyo Mganga PEPE AU PIERRE ana asili ya Haiti au visiwa hivyo vyenye ku practice voo doo.

HABARI NDIO HIYO!
 
Tausi mzalendo Voo Doo ndio nini??maana kuna nchi ukitaja hivyo wanajua hiyo ni vodka ingawa wao wanaita vodoo

Back
Top Bottom