Mapenzi kwangu bhasi

Joined
May 22, 2017
Posts
65
Reaction score
299
Hapa duniani tunapita tu hakuna atakayebakia ila milima peke yake, hivi mwanamke ni mtu au jini mtu? Kwanini wanajifanya wanabadilika kama rangi kwenye upinde wa mvua? Safari ya mapenzi kwangu imekuwa ndefu sana na natarajia kutooa tena maana wanawake wamekuwa nyundo kwa uongo kwa waume zao.......

Hivi mtu unampigia simu hapokei mara anakata halafu unaamua kunyamaza kimyaaaa baada ya siku kama tatu anakwambia simu iliibiwa baadaye anakwambia nataka kubadili simu hivi wanawake mmetuona sisi wanaume mataira au? Simu iliyoibiwa na inayobadilishwa ni ipi? Sikuongea neno hapo nikamwambia ukibadili unambie......Mpaka leo yupo kimya na anapatikana online everyday lakini si kwa sababu yangu anajua yeye..

........Eti leo ananipigia simu nimelazwa naumwa sasa mimi nimfanyaje? Wanadanganya mpaka wanaanza kusema ukweli kwenye uongo wao........ Mwingine siku hiyo nipo zangu misele mtaani akanipigia simu upo wapi, nikamwambia njiani naelekea kwangu akaniuliza maeneo gani nikamjibu karibu na kibao cha shule akanambia nimsubiri nikamwambia poa........

Nikakaa kabisa nikimsubiri baada ya muda nampigia ananambia eti nilishapita kwani bado upo hapo uliponambia? Nikamwambia ndio nipo hapa hapa wewe ulipitia wapi?Akakata simu mimi nikaondoka kwenda zangu gero kwangu nilipofika akanipigia tena na kunambia eti daddy wake alimpigia simu na kumuuliza upo wapi that why akanipita bila kuniona mimi nikam challenge na swali dogo tu....Kwani pale kama ungekuja ukaniona tulikuwa tunarudi nyuma au tulikuwa tunaenda njia moja kwenda kwenu na kwangu maana tupo jirani? Akakata simu nami nikamwandikia sms nikamwambia danganya watoto lakini si mimi mchaga ninayejua step zote au mdanganye mama yako na baba yako si mimi......

Nikamblock sasa hawa woote wanawake na wananisumbua sana na kila mmoja nishamwambia ruhusa nimewapa kutafuta mwanaume anayekufaa kama mimi sikufai niache......Lakini wananisumbua tuu kila siku niwafanyaje??????
Nimegombana nao nimechoka now nipo kimya tu ushauri plz ili nijue niwafanye nini mimi......
 
Relax ndugu, unatumia nguvu nyingi mno mwishowe unaumia. Usiwachukulie wanawake serious sana watakupasua kichwa kwa mawazo.

Na kama hivyo wakishakujua haupo imara ndio watakutikisa hadi ujihisi unapasuka. Mwanamke unatakiwa kuenda nae mdogo mdogo. Hizo principal zako za kidumedume hazi- apply kwao kila wakati,
 
Vizuri havitaki pupa vinataka SIMPO

So leo kesho kuanguka mi bado NIPO

Napata nnachotafuta nakosaje DIKO?

Ni mwendo wa kuvunja fupa mana meno IKO


(YOUNG KILLER ft Dully sykes & Ben Paul)[emoji121][emoji121]

Ushauri wangu[emoji116][emoji116]

Wewe una thamani kuliko huyo mpuuzi. Hivyo jipende mwenyewe tu inatosha.

Watakao kupenda watakuwa wa ziada


Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Ushatoa maamuzi ya kuwaacha kingine nini unataka wakati jibu unalo
 
[emoji23][emoji23][emoji23]yaani nilivoona tu hii post kabla hata sjaifungua nimecheka sana,,,,alafu we bado mdogo unataka vikubwa kuwa mpole dawa ikuingie[emoji382][emoji382]
 
Wanawake mambo mengi mkuu.. niruhusu nami nimgombeze Hawa kidogo!

Mimi toka Hawa ale tunda, imani nao ikaondoka kabisa.. yani alikosa nini bustani ilisheheni kila kitu kizuri!?
 
Njoo kwenye chama letu la CHAPUTA[emoji23][emoji23]
 
Unawatoa wapi wanawake wa aina hiyo?
 
Mkuu mbona na wewe mwenyewe huna msimamo, fanya maamuzi ya kiume acha kucheka nao kenge hizo
 
Mchaga wa wapi wewe unawaza wanawake badala ya kuwaza pesa
 
Kwa namna unavyoteseka nilitegemea utajiua au utajijeruhi kumbe porojo tu. Kama hupendwi si ufe. Kuna haja gani ya kuishi kwenye dunia ambayo hupendwi.

Kufa nenda ukaishi mbinguni kwa amani na hakuna mapenzi huko ni kuimba na kusifu.
 
Ina maana kwa wakati mmoja uko na Wanawake wawili au? naomba kueleweshwa hapa nimeshindwa kuelewa.
 
Jipende tu mwenyewe, wao waje kama extra tuu, don’t take them seriously, atatokea tu mmoja utaona ana fit ila by the time being FANYA MADA ZAKO TUU
Kabisa, wewe deal na mambo yako usiwaingize akilini kwa asilimia kubwa, utachoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…