Mapendekezo yangu juu ya katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapendekezo yangu juu ya katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by KAUMZA, Jan 1, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Haya ndo mapendekezo yangu kwa katiba mpya
  1. Ardhi iwe ni suala la kikatiba kama ilivyoshauriwa na Tume ya Issa Shivji mwaka 1992
  2. Kuwe na serikali 3 kama ilivyoshauriwa na Tume ya Jaji Kisanga/white paper
  3. Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU apewe kinga(security of tenure) kama ilivyo kwa majaji
  4. Cheo cha mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya vifutwe(kama sera ya CDM mwaka 2005)
  5. Matokeo ya urais yaweze kuhojiwa mahakamani
  6. Kuwe na tume huru ya uchaguzi
  7. Rais mstaafu aweze kufikishwa mahakamani kwa makosa aliyoyafanya alipokuwa Rais
  8. Mbunge aruhusiwe kugombea vipindi viwili tu na asirudietena
  9. Mgombea binafsi aruhusiwe ktk ngazi ya ubunge na udiwani tu
  10. Viongozi wa dini/waliowahi kuwa viongozi wa dini wasiruhusiwe kufanya siasa za moja
  kwa moja
  11. Mawaziri wasiwe wabunge
  12. Sera ya ujamaa isiwe sera ya taifa kama ilivyo katka ibara ya 3(1)
   
 2. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  weakleaks
   
 3. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  mapendekezo hayo KIKWETE HAWEZI KUPITISHA
   
 4. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,813
  Likes Received: 1,057
  Trophy Points: 280
  slaa je?
   
 5. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kama ni kiongozi wa dini au aliwahi kuwa kiongozi wa dini atakuwa amekumbwa na ufagio. Lengo langu hasa kuwa-exclude watu hawa(viongozi wa dini/waliowahi kuwa viongozi wa dini) ni kuondoa dhana ya wapiga kura kuwa huenda akapendelea watu wa aina fulani. In short, awe huru(with no bias)
   
 6. D

  DENYO JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Prof issa shivji kusaidiana na dr slaa wanafaa kuongoza tume ya katiba mpya
  Kama jk anataka kweli kuondoa fitina na kulitakia mema taifa hili-basi watu hawa wawili wanafaa kabisa kwa vyovyote na kwa maslahi ya umma kuongoza tume ya katiba mpya.

  1. Prof issa shivji amekuwa katika mchakato wa kudai katiba mpya kabla na baada ya mfumo wa vyama vingi. Sio mnafiki, hanunuliki kama wasomi wetu wengi -anayetaka ukweli asome raia mwema la wiki ya jana atapata ukweli huu kutoka katika makala yake. Hayumbishwi. Nampendekeza awe mwenyekiti wa tume hiyo

  2. Dr w. P. Slaa ni mtanzania mwenye msimamo aliyesababisha chachu ya katiba mpya, kama ilivyo kwa shivji slaa(phd) hanunuliki na hayumbishwi. Ni mtanzania aliyekuwa anagombea urais agenda yake kubwa ya kwanza ikiwa ni kuanzisha mchakato wa katiba mpya. Ni mtanzania anayeona mbali na anayeitakia mema nchi hii, mwenye kuchukizwa na umaskini, ufisadi, ujinga, na maradhi ya nchi. Huyu anafaa kuwa katibu wa tume hii -aombwe ashiriki hatakama yeye mwenyewe hakubaliani na approach ya serikali ya jk. Lakini kwa jk kumuomba na kumtumia katika tume hii wote wawili watakuwa wameweka historia ya aina yake kwa maslahi ya umma.

  Tunao watanzania wengine kama jaji kisanga,ulimwengu, ayoub lioba, amiri maneto, bomani -hawa wanaweza kutumika kama wajumbe pamoja na mama nkya, ila hoja kubwa ni kutaka watanzania wazalendo wa kweli -nilisikitishwa na tume ya bomani ya madini ambayo mpaka leo bado wizi wa madini unaendelea -ndio maana slaa(phd) hataki tume hizi kwa kuwa zinakuwa hazipo huru.

  Haya ni maoni yangu na ninaamini wapo wana jf watakubaliana na mimi kwa kupitia reference ya tume zilizowahi kuundwa huko nyuma na matunda yake. ​
   
Loading...