Mapendekezo ya Ramani ya Tanzania Bara Chini ya Sera ya Majimbo

Abba

Member
Joined
Jul 30, 2007
Posts
40
Reaction score
13
WanaJF

CHADEMA na baadhi ya wadau wengine (TGNP,Jukwaa la Katiba etc) wamependekeza kwenye Tume ya mabadiriko ya katiba kuingizwa katika katiba mpya kipengere kinachoweka utawala wa majimbo(states) na kuhainisha ni mikoa gani katika ramani ya sasa hivi inapashwa kufanya majimbo hayo. Hii ni hoja ambayo itakuwa moja ya hoja ambazo zitakuwa "controversal" hasa utakapofika uandikaji wa katiba yenyewe (kwa sababu hii ni mitazamo inayokinzana ya makundi mawili yenye nguvu, na waungwaji mkono)na vile vile kwenye kura ya maoni.

Mimi kama wanaJF nimeingalia kwa kina hoja hii na nifikiri hoja hii haiepukiki kwa sababu zifuatazo;
1.Kwanza Tanzania na nchi za Afrika Mashariki zipo kwenye mradi wa Afrika Mashariki ambao final product ni political federation. kwa nchi kubwa kama Afrika Mashariki, ni vigumu kuendesha nchi toka Arusha ( kama itakuwa ndiyo "Washington DC yetu" bila kuwa na regional administrations, kwa maani hii ni majimbo.

2.Hoja ya pili ni kwamba katika nchi ambayo inaendeshwa kwa misingi ya demokrasia viongozo wanachaguliwa na wananchi na kwa maana hiyo lazima wakuu wajimbo wachaguliwe na wananchi sio kutoka Ikulu (Arusha???).Kama hiyo haitoshi watani wetu wajadi (Kenya) katika katiba yao mipya wameweka utawala wa majimbo wa kuchaguliwa! na kuanzia Machi mwaka huu watakuwa na serikali zao za majimbo. Vile vile Rwanda nao wanaserikali za majimbo lakini bado wakuu wanachaguliwa na Rais.Kwahiyo sio rahisi kuingia katika Afrika Mashariki halafu tuwaambie waKenya na Rwanda wafute majimbo.

3.Hoja ya tatu ni kwamba katika katiba mpya ni lazima kuwepo na serikali katika kada ya kati, lakini kwa ukubwa wa nchi yetu na nia dhabiti ya kulinda umoja wa kitaifa na kupunguza gharama za uendeshaji si busara kugawa serikali za kada ya kati kwenye mikoa iliyopo sasa (23????). kwahiyo ni vigumu kukwepa serikali za majimbo. Baada ya kuangalia ramani Tanzania bara na maoni ya Chadema kuhusu magawanyiko wa Mikoa ya sasa kwenye majimbo napendekeza RAMANI YA TANZANIA CHINI YA KATIBA MPYA YENYE SERIKALI YA MAJIMBO PAMOJA NA MAKAO MAKUU YA MAJIMBO HAYO. Tofauti na Chadema walivyopendekeza kuwa na majimbo 9, mimi napendekeza majimbo 10 na makao makuu yao(states houses)kama ifuatavyo.
1.Jimbo la Nyanza Magharibi lenye mikoa ya Kagera, Geita na Shinyanga(Angalia ramani);
2.Jimbo la Nyanza Mashariki lenye Mwanza, Mara na Simiyu;
3.Jimbo la Kanda ya Nyanda za Juu lenye mikoa ya Njombe, Mbeya na Ruvuma;
4.Jimbo la Ziwa Tanganyika lenye mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa;
5.Jimbo la Kati Magharibi lenye mikoa Tabora na Singida;
6.Jimbo la Kati Mashariki lenye mikoa ya Dodoma na Iringa;
7.Jimbo la Kaskazini lenye mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro;
8.Jimbo la Pwani ya Kaskazini lenye mikoa ya Tanga, sehemu ya pwani na sehemu ya Morogoro (Angalia ramani);
9.Jimbo la Pwani ya Kusini lenye mikoa ya Ulanga, Lindi, Pwani na Mtwara (Angalia ramani);
10.Jimbo la Dar es Salaam. (hili libaki peke yake)

Katika ugawanywaji huu wa majimbo rasimali zifuatazo zitabaki chini ya serikali ya shirikisho (Tanganyika)
1.Barabara kuu ambazo zinaunganisha mikoa (ambazo sasa zipo chini ya TanRoads)
2.Bandari kwenye Bahari na maziwa
3.Airports (kubwa na size ya kati)
5.Rasilimali zozote zinazopatikana chini ya aridhi (Mafuta, Gasi na madini)kwa maana ya Licensing na kodi mauzo ya kampuni -Corporate tax

Najua zipo hoja ni nyingi na za mashiko lakini hizo hapo juu zitoshe kuanzisha mjadala.

Tujadili
 
Attachments

Yaani we bado unaamini kwamba tutakuwa nchi moja na wakenya? Duuh! Ngoja nikajimilikishe ekari zangu kijijini maana tunavyoendelea kutetea ardhi iwe mali ya wote, wengine mnataka kuwaleta na wakenya waje wamiliki sawa na sie wakati kwao hata jani hukati.
 
Good post. Nitarudi na hoja.
 
Back
Top Bottom