mapendekezo ya katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mapendekezo ya katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by jonjo, May 2, 2012.

 1. j

  jonjo New Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Dec 15, 2006
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  maoni ya mapendekezo ya katiba mpya
   
 2. m

  member2012 Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri tumeanza kupokea maoni, Nashauri na wengine wetu pia tutoe maoni yetu kwa mujibu tunavyotaka KATIBA yetu iwe.

  Bila ya shaka Mabadiliko ya KATIBA yetu ni lazima yatokana na mawazo yetu wenyewe,

  Ni vyema kama hatutosubiri mpaka Serikali ama tume watuletee mapendekezo
   
 3. k

  kidebe New Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Me naona wanaopokea maoni yafanyiwe kaz km yalivyo
   
 4. W

  Wamnetu Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi punde tu Mheshimiwa Rais amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri na idadi ya mawaziri pamoja na manaibu wao imeongezeka kufikia 55. Swali la kujiuliza ni kwamba ni kigezo gani alichotumia hadi akaongeza mawaziri kutoka 50 hadi 55. Kutokana na haya, ningependa katiba yetu iwe na yafuatayo:  • Idadi ya wizara iweke bayana kwenye katiba;
  • wanaobahatika kuteuliwa kushika madaraka serikalini - iwe mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa vyombo vya usalama, nk wapitishwe ma bunge la Muungano kabla hawajashika nyadhifa zao;
  • endapo gharama zitaruhusu, pawepo na bunge la kila mkoa ambalo litakuwa na wajumbe waliochaguliwa kutoka huko mkoani wanakotoka; hii ina maana kuwa wakuu wa Mikoa watachaguliwa katika vikao hivyo vya Bunge la Mkoa. Miongoni mwa shughuli zao za awali ni kuteua wasaidizi wakuu katika wilaya na kusimamia kikamilifu mapato na matumizi ya mikoa yao;
  • Nafasi za kuongoza mashirika ya umma zitangazwe na wenye sifa zinazohitajika wafanye kuomba na wafanyiwe usaili na baada ya hapo majina yafikishwe bungeni kupitishwa.
   
 5. M

  MWANAIDEA Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ยท[FONT=&quot] NAPENDEKEZA YAFUATAYO KATIKA KATIBA MPYA

  MIKATABA YOTE INAYOHUSU NCHI IPITIWE NA TUME/JOPO LA WATAALAMU ALAFU IPELEKWE BUNGENI KABLA YA KUSAINIWA NA RAISI.

  UWEPO WA MABUNGE MAWILI


  (I) BUNGE LA UWAKILISHI
  Hili ni bunge ambalo litatokana na kuchaguliwa kutoka kila wilaya ,na mbunge atakua mwenyekiti wa hamashauri husikahivyo basi kila wilaya itakuana mbunge mmoja .hii itasaidia kupunguza idadi kubwa ya wabunge , kuondoa mgongano wa madaraka kati ya mbunge na mkiti wa halmashauri, pia kuwa kiungo kati ya serikali kuu na serikali ya mitaa.yaani halmashuri.kwa mfano kwa sasa tungekua na wabunge133.Nafasi ya mkuu wa wilaya isiwepo majukumu yake yachukuliwe na mkurugenzi wa wilaya.
  (11)BUNGE LA WANANCHI
  Hili ni bunge litakalotokana na kila mwananchi kuwa na nafasi ya kushiriki ,kuchangia ,kupanga , na kuamua masuala ya kitaifa litakua na m/kiti na katibu wake hili ndilo litakua msingi wa maamuzina ushauri kwenye bunge la uwakilishi ,kila mtanzania atapata fursa ya kushiriki na kusema chochote atakachoona kinafaa ili kuimarisha taifa.linaweza likawa linafanyika kwamwaka mara tatu kwa mwaka kujadili mustakabali wa taifa,

  BARAZA LA MAWAZIRI

  baraza la mawaziri liwe ni chombo cha kiutendaji ,hivyo basi liundwe na wataalamu waliobobea ambao watakua ni watumishi wa wa umma nawatawajibika kwa bunge kwa utendaji wao.na watakua wanapewa malengo endapo watashindwa kufanikisha malengo hayo watatolewa kwenye nafasi zao ili kuondoa siasa zisizotekelezeka,

  USIMAMIZI WA FEDHA

  Usimamizi wa fedha uwe chini ya CAG na HAZINA, hazina watatakiwa kupeleka fedha zote kwakuingiza kwenye akaunti zinazohusikakama ni miradi,vijiji, shule,halmashauri au taasisi kupitia akaunti zao mkurugenzi wa wilaya atakua ni msimamizi tu hii ni kuondoa ubadhirifu wa fedha za umma.la msingi ni kuimarisha taasisi hizi.

  UWEPO WA TUME HURU YA UCHAGUZI

  Tume ya uchaguzi huru isiyofungamana na upande wowote,pia iwe na mamlaka ya kushitaki au kushitakiwa na mtu yeyote kikundi au taasisi yeyote,chama.

  IAINISHE VIPAUMBELE VYA TAIFA

  Katiba mpya inatakiwa kuainisha vipaumbele vya taifa,ili kila kiongozi au utawala utakaochukua madaraka ujikite kutekeleza vipaumbele hivyo.kwa upande wangu napendekeza teknolojia ndio kiwe kipaumbele namba moja.[/FONT][FONT=&quot][​IMG][/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
Loading...