Mapendekezo ya JK yatekelezwa UN, WHO

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
13495123_1126179114113212_8214712220416461303_n.jpg

Maoni yangu

Kweli nabii hakubaliki nyumbani, JK ni hazina ya taifa na dunia kwa ujumla, mungu amjaalie mwisho mwema.
 
Naona kiswahili kigumu jopo la ngazi ya juu au JK . Headline ya gazeti na content tofauti.
 
JK ni mtu na nyota yake baba hakuwa raisi wa kung'ang'ania bei ya chumvi
 
Naona kiswahili kigumu jopo la ngazi ya juu au JK . Headline ya gazeti na content tofauti.
Wewe ndo unaona tofauti-- hilo jopo lipo chini ya Uenyekiti wa JK; sasa huo utofauti wa headline na content upo wapi?!
 
Mwenyezimungu alimpa Karama za kipekee Jakaya! Hizi ni Taarifa mbaya sana Wafuasi wa Yule mwenye Tuzo ya Amani kutoka Makanisa 2000 ya shahidi wa Yehova na Ufufuo kutoka Lubumbashi.
 
Mwenyezimungu alimpa Karama za kipekee Jakaya! Hizi ni Taarifa mbaya sana Wafuasi wa Yule mwenye Tuzo ya Amani kutoka Makanisa 2000 ya shahidi wa Yehova na Ufufuo kutoka Lubumbashi.
KARAMA YAKE INANGARA DUNIANI KOTE HAKUNA WA KUIZUIA
 
Evil the evil ones have a good spirit sometimes, we can't be all good or all bad, we are both, good and bad!
 
Kiongozi bora ni yule aliye na maono ya kesho na kesho kutwa. Anaona mbali na kuchuja yale anayoyaogea na kujua mapema athari ya akitamkako. Ni mtu anayeheshimu mawazo na kutoa uhuru mpana wa watu kumsema ili kama kuna sehemu kakosea ajirekebishe. Pengine hili ndilo limemfanya aonekane bora kuliko wengine.
 
UMENENA VYEMA
 
Evil the evil ones have a good spirit sometimes, we can't be all good or all bad, we are both, good and bad!
kuna ukweli ndani ya hilo uliloandika nakubaliana na wewe,waswahili tuna sema mtu hata awe mbaya vipi lazima atakua na wema fulani hata kidogo tu. Yaani mbaya halisi na wema hakosi.
 
JK ni born Leader.
JK ni kama Mwalimu mkuu Siyo kama Mwalimu wa zamu
JK ni kama dereva siyo kama konda
JK ni kama mkuu wa gereza siyo kama Nyapara

Kikubwa sana kinachombeba huyu jamaa ni UTU, UBINADAMU nafsini mwake anao mwingi sana.
 
Wengi tutamkumbuka zaidi baadae..tofauti yake na huyu ni safari za nje..otherwise namuelewa sana.
 
'charity begins at home' MTANZANIA kwanza, mama TANZANIA kwanza
 
JK ni born Leader.
JK ni kama Mwalimu mkuu Siyo kama Mwalimu wa zamu
JK ni kama dereva siyo kama konda
JK ni kama mkuu wa gereza siyo kama Nyapara

Kikubwa sana kinachombeba huyu jamaa ni UTU, UBINADAMU nafsini mwake anao mwingi sana.
HUyoo sio kama yule mzee wa ''....Fukuza wote, na madarasa yao tutageuza mabanda ya kufugia kuku....'' Big up kijana wa msoga
 
Kuna watu wako interestingly unobjective, wakikuchukia basi hata ukifanya jambo jema kiasi gani ni either watafumba macho wasilione kabisa au watatafuta namna ya kulibeza kwa nguvu zote. I do not think this is right in any measure.

Kuhusu hili la JK, kimsingi kwa sisi tunaojua, hii ni accomplishment kubwa sana kama kiongozi. Kuna waoponda kuwa hakuwa yeye binafsi bali ni jopo aliloongoza. What difference does that make?? Ni dhahiri kuna shida ya uelewa hapa kuhusu dhana ya uongozi au ushabiki na political orientations zetu zinatu-blind....of which in my view that is a serious professional disaster and obviously has a huge negative implication on our overall development as a nation!

Hatutafika kwa utaratibu huu. Tubadilike!! Tupongezane inapobidi. Pia tukosoane na kurekebishana constructively kila inapolazimu.
 
Back
Top Bottom