Mapendekezo kwa Sekretarieti ya Ajira

Mapendekezo kwa Sekretarieti ya Ajira

Mimi nimeona na kuhakiki watu kadhaa wakipata kazi kupitia utumishi bila kumjua mtu, hilo naweza lisemea kwa kujiamini. Lakini hili la kusema nafasi zina watu au kuna vimemo n.k ni maneno ambayo siwezi sema huwa siyaskii vijiweni ila sijawahi yathibisha, inawezekana ikawa kweli au si kweli, si vyema kushikilia kitu bila kuthibitisha. Lkn kama anayesema nafasi zina watu anao uthibitisho basi ana haki ya kusema hvyo na ni vyema akasema kwa kutoa uthibitisho hapa.
 
Inawezekana kabisa sekretariet inakua na nia nzuri ila nia inapotea kwa kulazimishwa kufuata maelekezo ya wakubwa fulani ambayo husababisha utendaji wake kuchafuka, na ndio maana kinahitajika chombo huru ambacho si kwamba kitakua kinasikilza malalamiko tu bali pia kitailinda sekretariet na kuifanya iwe huru kiutendaji. Kwa mfano usahili wa National Audit Office (NAO), pale naweza kusema kwa uhakika kuwa sekretariet ilifanya makosa ya wazi japo hawawezi kiri, na inaonekana ilikua nje ya uwezo wao kuepuka walicho kifanya
 
yeah mi nakubaliana na mtoa mada.kweli bodi ya ajira naona bado hawajajipanga kwenye kada mbalimbali labda kwa kutojua .mfano uhasibu,bodi ya ajira hawatambui statement of result zinazotolewa na bodi ya uhasibu(NBAA) wanataka vyeti tu sio statement of result.Kwaiyo watu waliosoma mfumo wa bodi kuanzia ATEC1 mpaka INTERMEDIATE STAGE(module c&d), hawezi pata kazi wakati hao ni equivalent to degree ya uhasibu.
 
Kazi zipo omba na kuomba,ukisema kazi zinawenyewe na wakati kila leo watoto wa wakulima wanapata kazi
 
Inawezekana kabisa sekretariet inakua na nia nzuri ila nia inapotea kwa kulazimishwa kufuata maelekezo ya wakubwa fulani ambayo husababisha utendaji wake kuchafuka, na ndio maana kinahitajika chombo huru ambacho si kwamba kitakua kinasikilza malalamiko tu bali pia kitailinda sekretariet na kuifanya iwe huru kiutendaji. Kwa mfano usahili wa National Audit Office (NAO), pale naweza kusema kwa uhakika kuwa sekretariet ilifanya makosa ya wazi japo hawawezi kiri, na inaonekana ilikua nje ya uwezo wao kuepuka walicho kifanya

Walifanya nini?
 
Walifanya nini?

Watahiniwa walipewa ratiba ya kufanya written jmosi na oral j4 (kwa watakao faulu), ikajulikana hvyo katika tangazo lililowaita kwenye usahili. Lakini j2 usiku utumishi wakaongeza ratiba na kuweka mtihani wa practical ufanyike j3 asubuhi kabla ya oral j4. Ni mabadiliko ya ghafla ambayo walipaswa kuhakikisha wanatumia juhudi kuwajulisha walio faulu japo kwa sms, lkn wao waliweka tangazo kwenye website tu, ambapo tangazo lilikua na utata na ilikua usiku kwa watahiniwa kutafuta msaada wa maelezo ya tangazo. Yamkini watahiniwa walizembea mahali, lkn secretariet ilizembea zaidi. Kilichofuata wale wachache walioenda practical ndio waliruhusiwa kufanya oral, na wengi wao walisaidiwa ufafanuzi wa tangazo na ndg zao wanaofanya kazi secretariet ya ajira. Kwa wasio na ndg ni nani angewasaidia ufafanuzi usiku ule?
 
Hapo wote wana makosa mtu msomi anatakiwa awe na habar zinazoendelea ikiwa pamoja na kuchek web yao mara kwa mara hasa kama ndio umepiga pepa upande wa pili pia wana makosa walitakiwa wawajulishe japo kwa sms kwani sizani kama walikua wengi
Lakini mwisho wa habari ni nani anaeathirika ni aliefanya usaili so inabidi na sisi wengine tujifunze kutokana na hili kua mara kwa mara ni vizur kuchek website yao kama kuna kazi tuliziapply au hata kama tayar tumeshafanya pepa
 
tunashukuru kwa kazi ambayo sekretarieti ya ajira wamekua wakiifanya, japo mapungufu yapo lakini pia wamesaidia ajira za serikalini kufahamika wazi panapokua na uhitaji.
Lakini ingependeza zaidi kama pangekuwepo na chombo huru ambacho kinaikagua sekretarieti katika utendaji na utekelezaji wa shughuli zake; ili kuhakikisha taratibu, sheria na kanuni zinafuatwa. Chombo hiki pia kipewe mamlaka ya kusikiliza malalamiko yenye mashiko kwa watu ambao hawajaridhika na utendaji wa sekretarieti katika jambo flani au kwa ujumla, na kutengua maamuzi ya sekretarieti pale inapobidi, maana kadiri siku zinavyo songa mbele weledi wa sekretarieti unaonekana kushuka na inaonekana kufanya kazi kwa mazoea.
Hii itasaidia kuboresha mfumo wa ajira nchini hasa kupitia kwa sekretarieti na kupunguza madhaifu ambayo yamekua yakiumiza na kusikitisha sana haswa kwa "watoto wa wakulima".
Narudia tena kuishukuru na kuipongeza sekretarieti katika yale iliyofanikisha, na kwa yale madhaifu naamini uwepo wa chombo hicho utayapunguza.
Nawasilisha.
hawa utumishi wanavituko sana siku hizi,walitangaza nafasi ya mkurugenzi mkuu chuo cha taifa cha utalii na waliweza kushorlist watu sita, matokeo yake waliita watu wawili tu, mmoja akiwa mkurugenzi aliyemaliza muda wake na mwingine ni ni mwalimu wa hapohapi chuoni. Lakini habari za uhakika ni kwamba huyo mkurugenzi anahonga watu wa utumishi ili aletewe watu ambao hawana ushindani kwake au akikujua kwamba umeomba hiyo kazi na nitishio kwake basi atakutafuta na kukuhonga ili usionekane kwenye interview. Cha ajabu kingine ni kwamba hata majina ya walioitwa kwenye interview hayakuwekwe kwenye website yao. Kimsingi secretarieti ya ajira siyo ya kuitegemea sana.
 
Back
Top Bottom